[Latest Updates]: Kituo Kipya cha TGC Kujengwa Arusha

Tarehe : March 23, 2024, 9:06 a.m.
left

●Kuongeza udahili wa wanafunzi kutoka 180 mpaka 450.

● Kuwa kitovu cha uthaminishaji madini Afrika.

Na.Samwel Mtuwa - Arusha

SERIKALI kupitia Wizara ya Madini  inatarajia  kujenga jengo pacha la Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC) jijini Arusha ambalo litasaidia kuongeza udahili kutoka wanafunzi 180 hadi 450 kwa mwaka.

Hayo yamebainishwa na Kaimu Mratibu wa kituo hicho, Mhandisi Ally Maganga wakati akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari  kuhusu mradi wa  ujenzi wa jengo hilo.

Mhandisi Maganga amesema, jengo hilo litakuwa na miundombinu mbalimbali ikiwemo madarasa, makumbusho, masoko ya madini ya vito, karakana za uongezaji thamani madini, maabara za madini ya vito na bidhaa za usonara, ofisi na mabweni ya wanafunzi.

Amesema, jengo hilo litakuwa mahsusi kwa utoaji wa mafunzo ya kuongeza thamani madini ya vito , minada ya madini ya vito na maonesho ya madini.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals