[Latest Updates]: Wanawake STAMICO Wahamasisha Matumizi ya Nishati Safi Rafiki Briquettes

Tarehe : March 8, 2025, 3:16 p.m.
left

Watumishi Wanawake wa Shirika la Madini laTaifa (STAMICO) wametumia maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake kwa kuhamasisha matumizi
 ya nishati safi ya kupikia ya Rafiki Briquettes.

Lengo la hamasa hii ni kuwawezesha wanawake na wasichana  kutunza mazingira kwa manufaa ya vizazi vijavyo

Hayo yamesamwa na Afisa Rasilimali Watu  Mwandamizi wa STAMICO, Bi Leah Jericho wakati wa maandamano ya kusherehekea siku hii leo tarehe 8 Machi katika Viwanja vya Leaders Club Jijini Dar es Salam.

Bi. Leah amesema STAMICO inaendelea kuhamasisha matumizi ya nishati safi ili kutoa elimu na  kutumiwa na watu wengi zaidi.

Amesema STAMICO imeamua kupeleka nishati ya Rafiki Briquettes kwenye Maadhimisho ya siku hii kitaifa  Arusha  ili kuonesha kwa vitendo jinsi  inavyoweza kutumika kwa namna tofauti kulingana na mahitaji mahsusi.

"Nitoe hamasa kwa wanawake nchini hasa wale wanaotumia nishati chafu za kuni na mkaa unaotokana na miti kuchangamkia nishati hiyo inayopatikana kwa bei nafuu" alisisitiza Bi Leah

Ametumia fursa hiyo kuishukuru menejimenti ya STAMICO kwa kuendelea kutoa nafasi kwa wafanyakazi wanawake kushiriki katika uendeleshaji na usimamizi wa miradi mbalimbali.

Licha ya STAMICO kushiriki kitaifa huko Arusha kwa kuonesha shughuli mbalimbali za Shirika  sambamba na kutoa elimu ya matumizi sahihi ya Rafiki Briquettes,  imeshiriki pia katika mikoa ya Dar es Salam, Songwe na Dodoma ambako kuna ofisi zake

Kaulimbiu ya Maadhimisho haya ni  Wanawake na Wasichana 2025, Tuimarishe Haki, Usawa na Uwezeshaji"

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals