[Latest Updates]: Wananchi wa Kigoma Waneemeka na Uzalishaji wa Chumvi

Tarehe : April 8, 2023, 11:45 a.m.
left

 # Uzalishaji wa chumvi kwa mwaka 2023 unatarajiwa kuwa tani 60,000

# Ajira kwa wanawake zashamiri, fursa zitokanazo na madini zaendelea kuongezeka

Na Mwanahamisi Msangi, KIGOMA

Aprili 08, 2023

AFISA Madini Mkazi wa Mkoa wa Kigoma, Mhandisi Pius Lobe amesema kuwa uzalishaji wa chumvi katika mkoa huo umefungua fursa mbalimbali za maendeleo ikiwemo ujenzi wa miradi ya kijamii na ajira kwa wanawake.

Mhandisi Lobe ameyasema hayo kwenye mahojiano maalum ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kipindi maalum na makala ya kuelimisha umma kuhusu fursa na mchango wa Sekta ya Madini katika mkoa huo yaliyofanyika katika mgodi wa Nyanza Mines Ltd, Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma.

Akielezea fursa zilizopo katika Sekta ya Madini kwenye mkoa wa Kigoma zilizotokana na mgodi wa uzalishaji wa chumvi, Mhandisi Lobe amesema kuwa uwepo wa mgodi umezalisha ajira nyingi hususan kwa wanawake ambao wamekuwa wakifanya shughuli za kuvuna na kupaki chumvi kwenye vifungashio maalum ikilinganishwa na wanaume.

Akielezea mikakati ya ukusanyaji wa maduhuli unaofanywa na ofisi yake Mhandisi Lobe amesisitiza, "Jukumu letu kubwa ni kuhakikisha tunaongeza makusanyo ya Serikali ili kufikia malengo ambayo tumewekewa na Tume ya Madini ambapo hadi sasa tumekusanya zaidi ya shilingi bilioni moja kuanzia Julai 2022 hadi sasa ambazo ni sawa na asilimia 87 ya lengo,” amesema Mhandisi Lobe.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkazi wa Mgodi wa Nyanza Mines Limited, Bonny Mwaipopo amesema kuwa uwepo wa kiwanda hicho imekuwa ni fursa kwa wakazi wa Uvinza, ambapo wakati wa uzalishaji wa chumvi wanaajiri takribani watu 1000 wanaofanya shughuli ya kuvuna na kupakia chumvi kwenye magari na kupeleka kwenye kiwanda kwa ajili ya kusafishwa.

Ameendelea kusema kuwa uwezo wa uzalishaji wa chumvi unaofanywa na mgodi kwa mwaka ni tani 45,000 ambapo kwa mwaka 2023 wamejipangia kuvuna tani 60,000 za chumvi na kuuza ndani na nje ya nchi kama vile Burundi na Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo.

Naye Mkazi wa Uvinza, Salome Amos ameishukuru Serikali kupitia Tume ya Madini kwa kuhakikisha Sheria ya Madini na kanuni zake inatekelezwa hali iliyopelekea uboreshaji wa huduma za jamii hususan miundombinu ambapo kwa sasa wamejengewa kivuko kinachowavusha kutoka sehemu moja kwenda nyingine kufuata huduma za afya na kijamii.

“Mwanzoni tulikuwa tunapata shida ya kuzunguka umbali mrefu lakini tunashukuru mgodi kwani kivuko hiki kinatusaidia, hata mtu akiugua anavushwa haraka bila malipo yoyote na kwenda kupatiwa huduma.” amesisitiza Salome.

 

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals