[Latest Updates]: Waziri Mavunde, Waziri Mchengerwa Kukutana Kushughulikia Tozo za Halmashauri Kwenye Madini

Tarehe : Aug. 6, 2024, 2:19 p.m.
left

Ni Kufuatia Changamoto za tozo za Halmashauri zilizowasilishwa na wachimbaji Morogoro

Waziri Mavunde awapongeza Morogoro kuvuka lengo la makusanyo ya maduhuli

Serikali kuongeza nguvu ya Utafiti Morogoro

Wachimbaji wamshukuru Rais Samia kwa mashine za uchorongaji

Waziri wa Madini Mhe Anthony Mavunde amesema Wizara ya Madini imekubaliana na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kukutana na kutatua changamoto ya tozo zinazowekwa na Halmashauri kwa wachimbaji wa madini nchini.

Aliyasema hayo  Agosti 5, 2024 Mkoani Morogoro  wakati wa kikao na Wachimbaji wa Mkoa wa Morogoro kwa lengo la kusikiliza na kutatua kero za wachimbaji mkoani hapa.

“Nimesikiliza kwa umakini mkubwa kilio hiki cha tozo za Halmashauri na tozo nyinginezo kwa wachimbaji wadogo,kero hizi sio hapa tu zipo maeneo yote nchini," alisema Mavunde.

Aliongeza kwamba  maelekezo ya Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa kuzitaka Wizara hizo mbili kukutana ili kushughulikia suala hilo.

"Nataka niwahakikishe mimi na Mwenzangu Mhe. Mohamed Mchengerwa tumekubaliana kwamba mara baada ya ziara ya Mh. Rais Dkt. Samia Suluhu mkoani Morogoro tutaitisha kikao cha pamoja ili kushughulikia suala hili,".

Pia, Waziri Mavunde  alitumia fursa hiyo kuwahakikishia wachimbaji wa Morogoro kuhusu dhamira ya Rais Dkt. Hassan kuongeza nguvu kwenye eneo la utafiti wa madini  ikiwemo  Mkoa  Morogoro  kunufaika.

Mhe. Mavunde aliipongeza Ofisi ya Madini Mkoa wa Morogoro kwa kuvuka lengo la ukusanyaji maduhuli kufikia shilingi  bilioni 4.9 zaidi ya lengo lililowekwa la shilingi bilioni 4.2bn.

Akisoma risala kwa niaba ya wachimbaji, Mwenyekiti wa Chama cha Wachimba Madini Mkoa wa Morogoro(MOREMA) Dkt. Omar Mzeru,  alimshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa mashine za uchorongaji kwa wachimbaji  wadogo na kutumia fursa hiyo kumuomba Waziri wa Madini kushughulikia changamoto kubwa inayotokana na uwepo wa tozo nyingi zinatozwa na Halmashauri na Taasisi nyingine za Serikali kwakuwa zimekuwa zikiwarudisha nyuma kimapato wachimbaji wadogo.

Vision2030: MadininiMaisha&Utajiri

InvestInTanzaniaMiningSector

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals