[Latest Updates]: Serikali Imedhamiria Kuwaondoa Wachimbaji Wadogo Kwenye Uchimbaji wa Kubahatisha - Mavunde

Tarehe : Feb. 23, 2024, 8:28 p.m.
left

Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imedhamiria kuwasaidia wachimbaji wadogo kupata taarifa sahihi za maeneo yao ili kuwaondolea changamoto ya kuchimba kwa kubahatisha.

Ameyasema hayo leo katika Kijiji cha Utimbe, Kata ya Lupaso, Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara wakati wa Uzinduzi wa zoezi la eneo la majaribio la Utafiti wa kina wa miamba yenye viashiria vya madini (High Resolution Airborne Geophysical Survey) linalofanywa na Kampuni ya TUKUTECH LTD kwa ushirikiano na Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini (GST).

“Wachimbaji wengi wadogo wamepoteza mitaji na nguvu nyingi kwa kukosa taarifa sahihi katika maeneo wanayochimba," amesema Mhe. Mavunde.

Amesema kupitia Vision2030 Serikali inatarajia kulifikia eneo kubwa zaidi la nchi yetu kwa kufanya utafiti wa awali wa viashiria vya miamba yenye madini ili kuwaongoza kwa usahihi wachimbaji wa Tanzania.

Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amenunua mitambo 15 ya uchorongaji ambayo itawahudumia wachimbaji nchi nzima baada ya kuwa imepata taarifa za awali za viashiria ya miamba.

Kwa upande,  Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti Madini (GST) Dkt. Mussa Budeba amesema taasisi yake imejipanga vyema kutekeleza zoezi la utafiti wa kina wa madini kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kwa lengo la kufanya utafiti wa kina kwa asilimia 50 kwa eneo la Tanzania ifikapo mwaka 2030.

Akitoa maelezo ya awali, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya TUKUTECH LTD Mhandisi Tukupala Mussa Mwalyolo amesema kampuni yake ipo tayari kushirikiana na Serikali katika kutimiza lengo la utafiti wa kina wa madini nchini ili kuchochea ukuaji wa sekta ya madini na kwamba wapo tayari kufanya kazi na wachimbaji wadogo nchini ili kuwapatia taarifa sahihi za maeneo yao.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Masasi ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Mhe. Dkt. Stephen Mwakajumilo na Mbunge wa Jimbo la Lulindi Mhe. Issa Mchungahela wameipongeza Wizara ya Madini kwa mkakati wa utafiti wa kina katika eneo la Masasi kwa kuwa litasaidia kuongezeka kwa shughuli za kiuchumi, ajira na kuchochea maendeleo katika wilaya hiyo.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals