Tarehe : June 22, 2024, 2:38 p.m.
Tukio hilo limetokea nchini Geneva-Uswisi wakati Rais wa Bodi hiyo Mh: Helen Clerk (Pichani akiwa na MD STAMICO Dkt. Venance Mwasse) akifunga mkutano wa bodi hiyo ulioendeshwa kwa siku tatu. Ambapo alitangaza kuwa mkutano ujao wa taasisi hiyo utafanyika mkoani Arusha nchini Tanzania.
Katika mkutano huo Tanzania iliwakilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Dkt. Venance Mwasse kama Observer na kupewa Fursa ya kutoa wasilisho la namna STAMICO ikiwa ni taasisi ya umma/SOE inavyotekeleza taratibu na vigezo vinavyosimamiwa na taasisi hii (EITI) ya uhamasishaji na uwajibikaji katika kuvuna rasilimali madini.
Aidha katika Mkutano huo Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt. Mwasse alielezea jinsi serikali kupitia STAMICO inavyoendelea kulea na kurasimisha shughuli za wachimbaji wadogo nchini Tanzania na mkakati huo ulipokelewa kwa mtazamo chanya na wadau wa sekta hiyo hasa hasa uongozi wa Benki ya Dunia unaosimamia shughuli za uvunaji wa rasilimali madini, gesi na mafuta na kuahidi kusaidia jitihada za serikali.
Katika neno la shukurani Dkt. Mwase alisema “ Niheshima kubwa na nifaraja kwa sisi watanzania tumepata bahati mkutano huu kwa sasa umefanyika hapa Geneva ya Dunia na mkutano ujao utafanyika Arusha Tanzania ambayo ni Geneva ya Africa, From Geneva of the World to to the Geneva of Africa what a Coincidence!” Alisema Dkt. Mwasse.
Naye mwenyeji wa Tanzania nchini Uswis Mheshimiwa Balozi Dkt. Abdallah Possi ametoa hamasa kwa watanzania kuanza kujiandaa ili kunufaika ipasavyo na fursa hiyo ya Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano na kuendelea kusisitiza utayari wake juu ya kuhamasisha uwekezaji wa fursa mbalimbali zilizopo Tanzania hasa za madini ya kimkakati nchini Uswis.
Katika hatua nyingine, Naibu Mwakilishi wa kudumu UN Bi: Hoyce Temu ameipongeza STAMICO kwa kusema kwamba “Nimejifunza mambo mengi kuhusu STAMICO na jinsi walivyowapa kipaumbele Wanawake wanaojishughulisha na Masuala ya Madini kupitia Chama chao (TAWOMA), ambapo tumekubaliana na MD kushirikiana kuendeleza kundi hili kwa kuwatafutia masoko, wafadhili, mitaji na wawekezaji.
Mh Rais amefungua nchi na sasa ni kazi na Dawa… Visit Tanzania” hayo ameyasema Bi: Hoyce Temu ambaye ni Naibu Mwakilishi wa kudumu UN Geneva-Uswisi.
by: madini
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…
by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…
by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.
’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…
by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…
by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.