[Latest Updates]: Utunzaji Kumbukumbu na Nyaraka za Serikali Ndiyo Msingi Mkuu wa Taifa- Mahimbali

Tarehe : Sept. 13, 2023, 11:45 a.m.
left

#Awaahidi Watumishi wa TEITI kushughulikia maslahi yao ili kuboresha mazingira ya kazi

Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Kheri Mahimbali amesisitiza kuwa utunzaji wa kumbukumbu na Nyaraka za Serikali ndio msingi mkuu wa Taifa  katika uendeshaji wa shughuli zote za Taasisi.

Amesema hayo leo septemba 13, 2023, wakati akifungua mafunzo ya maadili katika utumishi wa Umma kwa watumishi wa Taasisi ya Uhamasishaji wa Uwazi na Uwajibikaji Katika Rasilimali Madini , Mafuta na Gesi asilia (TEITI), yanayofanyika kwa siku mbili  jijini Dodoma. 

Amesema kuwa, ana matumaini  kila mtumishi wa taasisi hiyo atapata uelewa kuhusu Kanuni na maadili ya  Utumishi wa Umma yatakayo mpelekea  kujua haki na wajibu wake wakati akitekeleza majukumu yake sehemu ya kazi.

“Ndugu Washiriki, kumbukumbu na Nyaraka za Serikali ndio msingi mkuu wa Taifa letu katika uendeshaji wa shughuli zote za Taasisi. Uzalishaji, utumiaji, utunzaji na uteketekezaji sahihi wa kumbukumbu na nyaraka za Serikali ni jambo la msingi na la kuzingatiwa na watumishi wote. Ni muhimu kufuata na kuzingatia miiko ya utunzaji wa kumbukumbu na nyaraka pamoja na kuzingatia usiri na utengano sambamba katika matumizi yake” amesema Mahimbali. 

“Ili Utumishi wa Umma uwe wenye ufanisi na wa kuheshimika. Watumishi wanapaswa kuzifuata Kanuni za Maadili ya Utumishi pamoja na kuwa na tabia na mwenendo unaozingatia Sheria, Kanuni na Miongozo katika Utumishi wa Umma" ameongeza Mahimbali. 

Katika hatua nyingine, Mahimbali amewaahidi watumishi wa TEITI kuwa Wizara itawaboreshea maslahi ili kufanya kazi katika mazingira bora na yenye hadhi ya utumishi ya umma.

Pia, akitoa salaam kutoka kwa  Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde, Mahimbali amesema kuwa waziri  anawasihi kuzingatia mafunzo hayo kwa kila mada itakayo tolewa na wataalam kutoka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma  ili kuongeza  ufanisi katika  utendajikazi wa kila siku.

Kwa upande wake, Kaimu Katibu Mtendaji wa TEITI, Mariam Mgaya amesema kuwa uwepo wa taasisi hiyo unasaidia wananchi kujua uwazi na uwajibikaji sambamba na kuziba mianya ya rushwa kwasababu wananchi wanakuwa na taarifa za kutosha kuhusu shughuli za uendeshaji na usimamizi wa rasilimali Madini, Mafuta na Gesi Asilia. 

Akizungumzia juu ya majukumu ya taasisi hiyo Mariam amefafanua kuwa TEITI inajukumu la kuweka mahusiano mazuri baina ya Serikali, Kampuni na Wananchi katika  sekta zote za rasilimali madini ,mafuta na Gesi asilia.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals