Tarehe : Nov. 26, 2018, 9:09 a.m.
Na Greyson Mwase
Leo tarehe 25 Novemba, 2018 Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko amefanya ziara katika Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi uliopo wilayani Kahama mkoani Shinyanga lengo likiwa ni kukagua shughuli za uchimbaji madini, kusikiliza na kutatua kero mbalimbali zinazoukabili mgodi huo. Katika ziara hiyo Naibu Waziri Biteko aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Anamringi Macha, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama, Anderson Msumba, Katibu Tawala wa Wilaya ya Kahama, Timothy Ndaya, Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Kahama, Mhandisi Abdulrahman Milandu, Afisa Mgodi Mkazi wa Mkoa wa Kahama, Modest Tarimo, Mkaguzi wa Migodi kutoka Tume ya Madini Mhandisi Frederick Mwanjisi,wataalam kutoka Wizara ya Madini, Tume ya Madini pamoja na waandishi wa habari.
Sehemu ya Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi uliopo katika Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga.[/caption]
Mara baada ya kufanya ziara na kupokea taarifa ya hatua za kufunga mgodi wa Buzwagi, Naibu Waziri Biteko alitoa maagizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na:- mgodi kuwasilisha upya mpango wa ufungaji wa shughuli zake kwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini ili aweze kuwasilisha kwenye Kamati ya Kitaifa ya Ufungaji wa Migodi kwa ajili ya kuidhinishwa ili utekelezaji wake uanze mara moja, pawepo na utaratibu wa kupitia upya kiwango cha fedha zilizotengwa kwa ajili ya ukarabati wa mazingira (rehabilitation bond) na kuweka mkakati wa kuhakikisha kuwa shughuli za kiuchumi za wakazi wanaozunguka mgodi huo haziathiriki na ufungaji wa mgodi husika.
Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Biteko aliutaka uongozi wa mgodi huo kufuata sheria na kanuni za ufungaji wa mgodi kwa wakati na kuepuka kufanya kazi kwa zimamoto.
Meneja Mkuu wa Migodi ya Dhahabu ya Buzwagi na Bulyanhulu, Benedict Buzunzu alisema kama mgodi wamepokea maelekezo na kuahidi kuwa watayafanyia kazi.
by: madini
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…
by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…
by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.
’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…
by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…
by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.