Tarehe : Sept. 22, 2023, 8:58 a.m.
●Tafiti za awali za jiolojia zimefanyika kwa asilimia 97
●Utafiti wa Jiokemia asilimia 23
●Utafiti wa Jiofizikia asilimia 16
Wachimbaji wa Madini wametakiwa kuchangamkia fursa za taarifa za utafiti wa Madini zinazofanywa na Wizara ya Madini kupitia Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) ili kuchimba kwa tija.
Hayo yamebainishwa leo tarehe 22 Septemba 2023 na Mjiolojia Mwandamizi Deogratius Oreku wakati akitoa taarifa kwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe alipotembelea Banda la Wizara ya Madini na Taasisi zake katika maonesho ya sita (6) ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea mkoani Geita.
Mapema baada ya kupata taarifa za maendeleo ya Sekta ya Madini , Naibu Waziri alitaka kufahamu kuhusu taarifa za utafiti ili kuwasaidia wachimbaji wadogo katika uchimbaji Madini.
Akifafanua kuhusu taarifa za utafiti zinazotolewa na Wizara kupitia machapisho mbalimbali , Oreku amesema kuwa Wizara ya Madini kupitia kitabu cha Mwongozo wa Wachimbaji Madini Wadogo kimekuwa msaada mkubwa kutokana na taarifa zilizochapishwa kuhusu hatua za utafutaji Madini.
Sambamba, na mwongozo huo Wizara kupitia Taasisi zake imefanya utafiti wa kina katika maeneo saba yaliyotengwa kwa ajili ya uchimbaji mdogo ambapo utafiti wa awali wa jiolojia umefanyika kwa asilimia 97, Jiokemia asilimia 23 na Jiofizikia asilimia 16 hivyo wachimbaji wadogo wanaweza kutumia taarifa hizo ili waweze kuchimba kwa urahisi na uhakika.
Maonesho ya sita ya Tekinolojia ya Madini kwa mwaka 2023 yanaongozwa na kaulimbiu inayosema " Matumizi Sahihi ya Teknolojia katika kuinua wachimbaji wadogo kiuchumi na kuhifadhi mazingira"
by: madini
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…
by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…
by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.
’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…
by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…
by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.