[Latest Updates]: Wananchi waaswa kushirikiana na Serikali

Tarehe : Dec. 28, 2017, 9:38 a.m.
left

Wananchi wanaoishi kwenye maeneo yanayozunguka eneo kilipokuwa Chuo cha Madini (MRI) Kampasi ya Nzega wametakiwa kushirikiana na Serikali kulinda miundombinu ya eneo hilo.

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (katikati) alipowasili kilipokuwa Chuo Cha Madini Kampasi ya Nzega kwa ajili ya kujionea mazingira ya eneo hilo. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Godfrey Ngapula na kulia ni Mratibu wa Kampasi hiyo, Mhandisi Abraham Rwakajungute.[/caption]

Naibu Waziri wa Madini. Stanslaus Nyongo alitoa wito huo Desemba 15 wilayani humo alipotembelea eneo lililokuwa linatumiwa kama Kampasi ya MRI Nzega na kujionea hali ya wizi wa vifaa mbalimbali.

Alisema dhamira ya Serikali ilikuwa ni kuwa na Kampasi mbili za Chuo cha Madini Dodoma (MRI) moja ikiwa ni hiyo ya Dodoma ambayo ni Kampasi Kuu na nyingine ya Nzega ambayo itajikita zaidi kwenye mafunzo ya vitendo lakini kutokana na hali ya usalama imekuwa ngumu kuiendesha kampasi husika.

Alisema, kwakuwa eneo hilo hivi sasa halitumiki baada ya wanafunzi kuhamishiwa katika Kampasi ya Dodoma, Serikali inatafakari shughuli ipi ifanyike ambayo itatumia majengo hayo yaliyokuwa yakitumiwa na Chuo.

Akimtembeza kuona hali ya kampasi hiyo, Mhandisi Abraham Rwakajungute ambaye ni Mratibu wa Kampasi, alisema Kampasi hiyo ilikuwa ikitumika kama Kambi ya Wafanyakazi wa Mgodi wa Resolute na ilikabidhiwa rasmi Desemba 12, 2014 kwa Chuo cha Madini Dodoma (MRI) na ilianza ikiwa na wanafunzi wapatao 120.

Aliongeza kuwa, kutokana na hali ya usalama kutoridhisha, ikiwemo baadhi ya wachimbaji wadogo kuvamia kwenye maeneo yanayozunguka eneo hilo, ili kufanya shughuli za uchimbaji, ilibidi Kampasi hiyo ifungwe na kwamba wanafunzi walihamishiwa kwenye Kampasi Kuu ya Dodoma.

“Hali ya usalama hapa siyo ya kuridhisha, tumekuwa tukivamiwa mara kwa mara na huku baadhi ya vifaa muhimu vikiibiwa,” alisema.

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (wa pili kulia) alipofanya ziara ya kilipokuwa Chuo Cha Madini Kampasi ya Nzega. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Godfrey Ngapula.[/caption]

Naibu Waziri Nyongo aliwataka wananchi wa vijiji jirani na eneo hilo kushirikiana na Serikali kuwabaini wenye tabia ya kuvamia na kufanya wizi kwenye eneo hilo lililokuwa Chuo.

Aidha, alisema amepokea maombi ya wananchi wa vijiji hivyo ya kutaka kupewa maeneo kwa ajili ya kufanya shughuli za uchimbaji na alisema kuwa mara Tume ya Madini itakapoanza kazi maombi hayo yatashughulikiwa.

Eneo la Chuo cha Madini Kampasi ya Nzega lilijengwa na Mgodi wa Resolute na hapo awali lilikuwa likitumika kama Kambi ya Wafanyakazi wa Mgodi huo.

Imeandaliwa na:

Mohamed Saif,

Afisa Habari,

Wizara ya Madini,

5 Barabara ya Samora Machel,

S.L.P 2000,

11474 Dar es Salaam,

Simu: +255-22-2121606/7, Nukushi: +255-22-2121606,

Barua Pepe: info@madini.go.tz,                                                                               

Tovuti: madini.go.tz

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals