[Latest Updates]: Wizara ya Madini, Kampuni ya Faru Graphite Wajadili Maendeleo ya Mradi

Tarehe : July 6, 2024, 11:01 p.m.
left

Dodoma

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Msafiri Mbibo Julai 5, 2024 aliongoza kikao kati ya Wizara na Kampuni ya Faru Graphite Corporation kilicholenga kujadili maendeleo ya mradi wa uchimbaji madini ya Kinywe (graphite)  katika eneo la Mahenge Wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro.

Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika  jijini Dodoma, Mbibo aliihakikishia kampuni hiyo kushughulikia changamoto inazokabiliana nazo kwa kushirikiana na mamlaka nyingine zinazohusika moja kwa moja  na masuala yatakayowezesha utekelezwaji wa mradi husika ili kuuwezesha kutekelezwa kwa wakati.

 Faru Graphite corporation ni kampuni ya ubia kati yake na Serikali ya Tanzania ambapo Serikali ina umiliki wa hisa zisizofifishwa za asilimia 16 na kampuni ya Black Rock Limited yenye hisa asilimia 84

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Faru Graphite Corporation John de Vries alieleza kwamba, katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita kampuni hiyo imeweza kushughulia masuala muhimu ikiwemo upatikanaji wa fedha kwa ajili ya ujenzi na uendeshaji wa mradi ili kuhakikisha unatekelezwa kwa wakati.

Pia, de Vries alitumia fursa hiyo kuishukuru Wizara ya Madini kwa ushirikiano inaoutoa katika kutatua changamoto zinazoikabili, na kuongeza kwamba, Wizara imesaidia kufikia makubaliano kati ya kampuni hiyo na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) ya ujenzi wa miundombinu na usambazaji wa umeme katika eneo la mradi.

#InvestInTanzaniaMiningSector

#Vision2030: MadiniMaisha&Utajiri

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals