[Latest Updates]: Hanang Yadhamiria Kuwekeza Kwenye Madini Ujenzi

Tarehe : July 4, 2024, 10:24 p.m.
left

Halmashauri ya Wilaya ya Hanang iliyopo Mkoani Manyara imedhamiria kuwekeza kwenye Madini ya Ujenzi hususan kokoto ili kuongeza vyanzo vingine vya mapato.

Hayo yamebainishwa leo Julai 04, 2024 na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Teresa Irafay baada ya kutembelea banda la Wizara ya Madini katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa ya  Dar es Salaam (DITF) maarufu kama Sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam. 

Amesema kuwa, maeneo mengi yaliyopo ndani ya Halmashauri hiyo yana miamba inayotumika kama kokoto ambayo wananchi wengi wamekuwa wakijishughulisha na uchimbaji wa kokoto lakini Halmashauri imeona hiyo kama fursa ya kuwekeza ili kuongeza vvyanzo vingine vya mapato.

“Halmashauri yetu hivi sasa tunategemea shughuli za kilimo, ufugaji, utalii, misitu kwa asilimia kubwa, ila tunataka tuanze kuwekeza katika madini ujenzi ambayo tunayo kwa wingi sana katika maeneo yetu” amesema Irafay.

Kwa upande wake, Mhandisi Migodi kutoka Wizara ya Madini Neema Mwafumbila amemueleza Mkurugenzi huyo kuwa, Halmashauri hiyo inapaswa kuomba Leseni kwa ajili ya kuchimba Madini hayo ya Ujenzi na baada ya kupata leseni hiyo Halmashauri itakuwa na uwezo wa kutafuta Mwekezaji na kuingia nae ubia na kuwa chanzo cha mapato.

Amesema kuwa shughuli zote za uchimbaji wa madini kwa uhalali zinahitaji leseni kutoka Tume ya Madini kwa kufuata utaratibu maalum uliwekwa kwa mujibu wa Sheria ya Madini.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals