[Latest Updates]: Prof. Msanjila Asisitiza Kuzingatiwa kwa Muongozo wa Uendeshaji wa Rush

Tarehe : Nov. 24, 2020, 12:01 p.m.
left

Na Issa Mtuwa – Bariadi Simiyu

Imeelezwa kuwa, migogoro inayojitokeza kwenye Rush (Mlipuko wa Madini) unasababishwa na Kikundi kinachoteuliwa kusimamia uendeshaji wa Rush zinazoanzishwa katika maeneo mbalimbali. 

Hayo yamesemwa Novemba 23, 2020 na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila alipotembelea kutatua mgogoro wa Rush ya Bulumbaka ulipo Bariadi mkoani Simiyu ambapo kuna mgogoro kati ya vikundi vya wachimbaji wadogo wa  Mwananyanzala Mine Group, Umoja ni nguvu, Ubunifu & Bulumbaka, Nyamagana Mine Group na Nguvu Moja Mine na mgogoro kati ya wachimbaji wadogo na wamiliki wa mashamba katika mkoa Simiyu wilaya ya Bariadi.

 “Rush ikitokea kikundi kilichoteuliwa kinatakiwa kizingatie miongozo, nini kifanyeki kwa wakati gani. Mambo yanayo fanyika kwenye mgodi wanaosimamia wamepewa mamlaka ya kusimamia kwa niaba ya Tume ya Madini kwa kuzingatia miongozo”, alisema Prof. Msanjila.

Alisema migogoro inayojitokeza inahusu mvutano wa vikundi vya wachimbaji wadogo wakitaka kila kikundi kiwe msimamizi wa Rush, mgogoro mwingine huibuka kati ya wachimbaji na wamiliki wa  mashamba ambayo madini yameibuliwa na mgogoro mwingine wa mgao unaotokea kati ya wachimbaji na wenye mashamba na mrahaba unaotolewa kwa serikali. Alisistiza muongozo kuzingatiwa kwa kuwa kilakitu kinacholeta mgogoro umetoa maelekezo.

“Someni muongo huu, unaonyesha kila kitu katika hayo mliyoyasema kila kitu kimewekwa wazi na ungefwatwa muongozo huu migogoro isingejitokeza”, aliongeza Prof. Msanjila.

Bwana Majuma Nzige ambae ni mchimbaji alisema chanzo cha mgogoro ni uongozi wa mgodi ambao unaosimamia shuguli mgodini apo. Ameongeza kuwa hata asilimia 30 wanazotozwa wahaoni kitu kinachofanyika huku bwana Webiro Kihatala alisema, pamoja na kuwa na msimamizi, mazingira ya mgodi sio salama kwa maana mazingira ni machafu hakuna vyoo lakini pesa wazotoa.

Kwa upande wa wamiliki wa mashamba, Ngila Machimu, alisema mgogoro wao na washimbaji wadogo wanachimba kwenye mashamba yao bila kupata faida na mazingira yao kwenye mashamba yanakuwa machafu kwa sababu hakuna vyoo.

Akijibu hoja zao kwa ujumla, Prof. Msanjila alisema suluhisho nililolisema ni uzingatiwaji wa muongozo na kutii. Kila kilicholalamikiwa muongozo unatoa suluhisho. Alisisitiza kwamba msimamizi atakae teuliwa hapaswi kuwa mchimbaji katika eneo analosimamia na lazima atoke na ndani ya mkoa wa Simiyu.

“Naagiza mchakato wa kumpata msimamizi wa Rush hii, uanze upya na azingatie muongozo katika kutekeleza majukumu. Wakati tukisubiri msimamizi mpya huyu aliyopo ataendelea kusimamia ili kazi ziendelee” alisema Prof. Msanjila.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals