[Latest Updates]: Waziri Mavunde Aridhishwa na Maendeleo ya Ujenzi wa Jengo la Wizara Mtumba

Tarehe : Aug. 9, 2024, 4:13 p.m.
left

Ataka Libebe Taswira ya Madini

Dodoma

Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde amesema kuwa ameridhishwa na Maendeleo ya Ujenzi wa  Mradi wa Jengo la  Makao Makuu  ya Wizara ya Madini unaoendelea katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma na kwamba, matarajio yake ni kuona mradi huo unaotekelezwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) unakamilika kwa wakati.

Ameyasema hayo leo, Agosti 9, 2024 alipotembelea mradi huo ili kukagua maendeleo yake ambapo amempongeza Mkandarasi kwa juhudi anazoendelea kuzifanya ili kuhakikisha jengo hilo linakamilika kwa muda uliopangwa.

Aidha, Mhe. Mavunde amewataka Mkandarasi huyo pamoja na Mshauri Elekezi  ambaye ni Wakala wa Majengo Tanzania (TBA)  kukamilisha jengo ndani ya muda uliopangwa ili Wizara iweze kutoa huduma kwa haraka na ufanisi kwa wadau kutokana na kupatikana kwa ofisi zote sehemu moja.

"Nawapongeza Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Wizara kwa siku za hivi karibuni kumekuwa na mabadiliko makubwa sana na mmezingatia ubora tulioutaka,’’amesema Mhe. Mavunde.

Pia, Waziri Mavunde amemhakikishia Mkandarasi na Mshauri elekezi kuwa Wizara itahakikisha inatimiza wajibu kwa upande wake ili kuhakikisha taratibu zote zinakamilika kwa haraka ili kuacha shughuli za kiufundi zikikamilika.

Katika hatua nyingine, Mavunde  ameitaka Menejimenti ya Wizara na mkandarasi  kuangalia namna ya ambayo itawezesha  jengo hilo  kubeba taswira ya Wizara  ya Madini  ambayo inakwenda sambamba na shughuli za Sekta ya  Madini, na kuongeza "tunataka kuona utambulisho utakaoonyesha kuwa hapa ndiyo Wizara ya Madini,’’ amesisitiza Waziri Mavunde.

Naye, Mshauri Elekezi kutoka TBA Msanifu wa Majengo Weja Ng’olo amesema wana imani kubwa na Mkandarasi kukamilisha ujenzi huo kwa wakati kutokana na kuwasili kwa vifaa muhimu vitakavyowezesha kuendelea na hatua nyingine za ujenzi

Kwa upande wake, Mkandarasi kutoka (NHC), Mhandisi Peter Mwaisabula amesema Shirika litahakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati.

Ujenzi wa Jengo la Wizara lenye ghorofa tano (5) unagharimu kiasi cha Shilingi bilioni 22. Hadi sasa ujenzi wa jengo hilo umefikia asilimia 84.4.

#InvestInTanzaniaMiningSector
 
#Vision2030: MadininiMaisha&Utajiri

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals