[Latest Updates]: Waziri Mavunde Aagiza Leseni za Utafiti 45 Mkoani Rukwa Kurejeshwa Serikalini

Tarehe : July 17, 2024, 12:23 p.m.
left

-Ni Leseni ambazo hazifanyiwi kazi na kuzuia maelfu ya wachimbaji kuchimba

-Eneo lililorejeshwa la ekari 812,383 ni kubwa zaidi ya Wilaya ya Sumbawanga

-Wachimbaji wadogo na wawekezaji waliotayari kupewa kipaumbele kwenye ugawaji

-Serikali kuchochea shughuli za uchimbaji madini mkoani Rukwa

Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde amesema Serikali imefuta na kuzirejesha Leseni za Utafiti wa Madini 45 kati ya 102 zilizopo mkoani Rukwa kwa kushindwa kufanyiwa kazi na kukidhi masharti yaliyowekwa.

Waziri Mavunde aliyasema hayo Julai 16, 2024 Wilayani Sumbawanga, wakati akijibu hoja za Uongozi wa Wachimbaji mkoani Rukwa kuhusu ombi la kupatiwa maeneo ya uchimbaji katika kikao kilichofanyika baina ya Waziri wa Madini na wadau wa Sekta ya Madini mkoani humo.

“Mhe. Rais Dkt. Samia S. Hassan ametupa maelekezo bayana ya kuhakikisha Leseni zinatolewa zinafanya kazi na watu wasihodhi maeneo makubwa bila kuyafanyia kazi ili kuchochea shughuli za uchimbaji na ukuaji wa sekta ya madini. Hapa Mkoani Rukwa tumerejesha Leseni 45 Serikalini ili kutoa fursa kwa Serikali kuyapanga vyema maeneo hayo kwa kutenga Leseni kwa ajili ya wachimbaji wadogo na wawekezaji wakubwa walio tayari kuwekeza kwenye sekta ya madini.” alisema Mhe.  Mavunde. 

Aliongeza kuwa, Leseni hizo 45 zilikuwa zimeshikilia eneo kubwa la ekari 812,383 ambalo ni kubwa kuliko eneo lote la Wilaya nzima ya Sumbawanga ambayo ina eneo la ukubwa wa ekari 667,641.

Vilevile, Waziri Mavunde alisema kuwa shughuli za uchimbaji mkoani Rukwa bado zipo chini, na kwamba ni jukumu la Ofisi ya Afisa Madini Mkoa kuhakikisha inachochea shughuli za uchimbaji  mkoani humo.

Kwa upande wake, Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Joseph Kumburu alimuhakikishia Waziri Mavunde kuwa atasimamia utekelezaji wa maagizo hayo hasa la kuchochea shughuli za uchimbaji wa madini  kwa kuwa Rukwa imejaaliwa madini mengi ya aina tofauti tofauti na kwamba una fursa kubwa ya kufanya vizuri zaidi. 

Awali, akiwasilisha taarifa ya Wachimbaji, Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji Mkoani Rukwa (RUREMA) Masie Mwambegele aliiomba Serikali kuwapatia maeneo Wachimbaji Wadogo katika maeneo ambayo hayafanyiwi kazi na kuomba Serikali kuongeza nguvu kwenye eneo la utafiti ili wachimbaji wasichimbe kwa kubahatisha kama ilivyo sasa.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals