[Latest Updates]: Tanzania Iko Tayari kwa Wawekezaji Sekta ya Madini - Dkt. Kiruswa

Tarehe : Feb. 8, 2024, 8:07 a.m.
left

 

Cape Town

Sekta ya Madini imezidi kuihakikishia Dunia utayari wa Tanzania kiuwekezaji kutokana na utajiri wa Kijiolojia unaobeba madini ya aina zote ikiwemo Mazingira rafiki kama Sheria, Kanuni na Miundombinu muhimu  inayochochea shughuli za madini.

Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa ameyasema hayo wakati wa mahojiano maalum na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya kimataifa kwenye Mkutano wa Uwekezaji wa Mining Indaba unaoendelea nchini Afrika Kusini katika jiji la Cape Town ambapo kwa mara ya kwanza, Tanzania inashiriki pamoja na Sekta binafsi kupitia Chemba ya Migodi Tanzania.

Ameongeza kuwa, bado Sekta ya madini Tanzania inahitaji wawekezaji katika maeneo mbalimbali ikiwemo teknolojia zinazotumika kwenye uchimbaji,  shughuli za utafiti wa madini na kusema   Tanzania imefanyiwa utafiti wa kina kwa asilimia  16  tu na kwamba  bado  zipo fursa nyingi kwenye eneo hilo.

 Aidha, ameyataja maeneo mengine kuwa ni pamoja na uongezaji thamani madini ambapo amesema eneo hilo  pia lina fursa za kutosha kutokana na Sera yaTanzania kusisitiza madini kuongezwa thamani nchini kabla ya kusafirishwa nje  kuanzia madini ya vito na mengine ikiwemo madini mkakati.

Aidha, Dkt. Kiruswa amefafanua kuwa, mabadiliko mbalimbali ya kisheria yaliyofanywa kwenye Sekta ya madini yalilenga kuiimarisha Sekta ya Madini na kuhamasisha ushiriki wa watanzania ili pande zote zinufaike.  
 "Tunawahakikishia wawekezaji usalama, faida, na wakati wote Tanzania iko tayari kuwahudumia na kufanya kazi pamoja. Zipo kampuni kubwa zimewekeza nchini kwenye Sekta ya Madini na pasipo shaka kampuni hizo hazijutii kufanya kazi Tanzania. Mfano mzuri ni mradi wa Kabanga Nikeli ambao unatarajia kuwa mradi mkubwa duniani katika uchimbaji na uchakataji madini mkakati ambayo yanahitajika sana duniani Kwa sasa,’’ amesisitiza Dk.Kiruswa.

Mkutano wa Mining Indaba ni moja ya mikutano mikubwa barani Afrika ambao unawaweka pamoja Serikali kutoka nchi mbalimbali, taasisi binafsi wawekezaji, wafanyabishara, wachimbaji na Wadau wengine yote ikiwa ni kuhakikisha rasilimali madini inazinufaisha nchi hizo. Katika mkutano huo nchi zinapata wasaa wa kushiriki midahalo, kutangaza fursa na kukutana ana kwa ana na wadau wenye nia ya kuwekeza na kupata taarifa za kina kwenye fursa wanazolenga kuwekeza.

Mwaka huu mkutano Indaba umetimiza miaka 30 tangu kuanzisha kwake ambapo umehudhuriwa na washiriki wapatao 8,100, wawekezaji 900, watendaji wakuu wa kampuni za Madini 700, na wakuu wa kampuni ndogo 470.

#TANZANIA@TheMiningIndaba2024         #InvestInTanzaniaMiningSector

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals