[Latest Updates]: Stamigold Watakiwa Kutafsiri Maono 2030, Madini ni Maisha na Utajiri kwa Vitendo

Tarehe : Sept. 21, 2023, 8:54 a.m.
left

 

#Dkt. Kiruswa awataka kupima sampuli zao katika maabara ya GST

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameutaka Mgodi wa STAMIGOLD kutafsiri kaulimbiu ya Wizara, Maono 2030; Madini ni Maisha na Utajiri kwa kuongeza bidii na ufanisi katika shughuli za uzalishaji wa madini ya dhahabu katika mgodi huo.

Amesema hayo leo Septemba 21, 2023 wakati akizungumza na wafanyakazi wa Mgodi wa STAMIGOLD uliopo Wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera akiwa katika ziara ya kukagua shughuli za Sekta ya Madini katika Mikoa ya Kagera na Geita. 

“Kwa kutambua na kuthamini kazi ya mtangulizi wake ambaye kwa sasa ni Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko, Waziri wetu Mhe. Anthony Mavunde na Wizara kwa ujumla  tumekuja na mkakati wa miaka 7, ambao kaulimbiu yake ni Maono 2030; Madini ni Maisha na Utajiri. Lengo hasa kuja kuyaendeleza mazuri yaliyopo ili kuhakikisha tunafikia malengo ya Sekta ya Madini katika maendeleo ya uchumi na hatimaye Pato la Taifa, tunaomba mkatafsiri hili kwa vitendo, ongezeni bidii na ufanisi” amesema Dkt. Kiruswa. 

Vilevile, amelipongeza Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kwa kazi nzuri ya uwekezaji katika miradi ikiwemo Mgodi huo na kwamba lengo la Serikali ni kuhakikisha Shirika hilo linakuwa miongoni mwa Mashirika ya Serikali yenye nguvu barani Afrika katika Sekta ya Madini. 

Katika hatua nyingine, Dkt. Kiruswa ameitaka STAMIGOLD kuihusisha Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) katika kutathmini sampuli zao na kwamba hakuna sababu ya kwenda kwenye maabara nje ya nchi wakati GST wanayo maabara katika mkoa wa jirani wa Geita.

Kwa upande wake, Kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi wa STAMIGOLD,  Mhandisi Rashid Lulanga  amesema kuwa katika kipindi cha Julai 2014 hadi Juni 2022 mgodi huo umefanikiwa  kuzalisha na kuuza jumla ya wakia 115,444.53 za madini ya dhahabu na wakia 15,405.54 za madini ya fedha, zote kwa pamoja zikiwa na thamani ya shilingi bilioni 362.2.

Ameongeza kuwa Mgodi umendelea kutoa ajira kwa Watanzania ambapo mpaka sasa jumla ya ajira 579 ikijumuisha watumishi walioajiriwa na mgodi moja kwa moja, watoa huduma na kandarasi mbalimbali na pia mgodi umeongeza muda wa mikataba ya kazi kwa wafanyakazi kutoka mwaka 1 hadi miaka 4 kuanzia tarehe 1 Aprili, 2022.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals