[Latest Updates]: Wabunge Wapongeza Maendeleo Sekta ya Madini Nchini

Tarehe : Feb. 10, 2024, 8:09 a.m.
left

 

●Serikali kuongeza mitambo kumi ya uchorongaji miamba.

●Asilimia 100 ya nchi ina taarifa za Jiofizikia (Low Resolution)

●Mikoa mitano tayari yafaidika na mitambo kuchoronga miamba.

Dodoma

Wabunge ambao ni wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Nishati na Madini wamepongeza maendeleo ya Sekta ya Madini kwa kufanikisha na kukamilisha miradi mbalimbali inayosimamiwa na Wizara ya Madini chini ya Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) pamoja  na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO).

Hayo yamebainishwa leo Februari 10, 2024 jijini Dodoma na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mathayo David Mathayo wakati akifunga  semina iliyotolewa na GST pamoja na STAMICO kuhusu utekelezaji wa  miradi ya maendeleo hususani  katika tafiti za madini zinazofanywa na taasisi hizo.

Akitoa ufafanuzi juu ya mada mbalimbali zilizowasilishwa, Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde amesema kuwa mpango wa Serikali kupitia taasisi ya GST ni kwamba ifikapo mwaka 2030 ni kufanya utafiti wa kina ili kufikia  asilimia 50  tofauti na asilimia 16 zilizopo sasa.

Mhe. Mavunde amefafanua kuwa, tayari maeneo matatu ya Lindi, Mtwara na Mirerani  yametengwa yenye ukubwa wa kilomita za mraba 165548 ambapo utafiti wa kina ukifanyika utaongeza asilimia na kufikia 34.

Naye, Mtendaji Mkuu wa GST Dkt.Mussa Budeba amesema kuwa taarifa zinazotokana na  utafiti unaofanywa na  GST zinagusa sekta mbalimbali kama vile sekta ya Maji, Afya, Kilimo, Ujenzi, Nishati safi, Utalii wa kijiolojia na mipango miji.

Kwa upande  wake, Mkurugenzi Mkuu wa STAMICO Dkt. Venance Mwasse  amesema Serikali ina mpango wa kuongeza mitambo mingine kumi ili kufikia lengo la mitambo 15 ya uchorongaji miamba itakayo ongeza tija kwa wachimbaji wadogo wa madini na kuwawezesha wachimbe kwa uhakika.

Akielezea kuhusu mitambo mitano ya awali Dkt. Venance amesema tayari imeshaanza kufanya kazi kwenye maeneo ya Nyamongo-Mara, Lwamgasa-Geita, Nhori-Dodoma na Itumbi Chunya.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals