[Latest Updates]: Rais Samia Ameiheshimisha Sekta ya Madini

Tarehe : Aug. 31, 2022, noon
left

Sekta ya Madini iko salama chini ya Rais Samia*

Mchango wa sekta hiyo waongezeka mpaka kufikia asilimia 7.9 kwenye Pato la Taifa*

Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko amesema Sekta ya Madini ipo salama chini ya Uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu.

Hayo yamebainishwa na Dkt. Doto Biteko wakati wa hafla ya Ununuzi wa Madini ya Tanzanite iliyofanyika mwishoni mwa juma katika Kituo cha Tanzanite Mirerani wilayani Simanjiro mkoa wa Manyara.

Dkt. Biteko amesema, Rais Samia Suluhu ameikuta Sekta ya Madini ikikusanya maduhuli ya serikali ya kiasi cha shilingi bilioni 475 ambapo ameipeleka sekta hiyo mpaka kufikia makusanyo ya bilioni 623 katika kipindi kifupi.

Aidha, Dkt. Biteko alisema, Rais Samia Suluhu ameikuta Sekta ya Madini ikichangia asilimia 5.7 kwenye Pato la Taifa na kuipeleka mpaka kufikia mchango wa asilimia 7.9 ambapo pia ameiwezesha sekta hiyo kujifungamanisha na uchumi wa sekta zingine.

“Wawekazaji wengi wamekuja kuwekeza kwenye Sekta ya Madini, tutafungua migodi mipya mitatu lakini vilevile refinery mbili kubwa zimejengwa na tunajenga refinery nyingine kwa ajili ya Nikel katika mji wa Kahama," amesema Dkt. Biteko.

Pia, Dkt. Biteko amesema kuwa, Taasisi na Kampuni mbalimbali zimekuja nchini kufanya tafiti ambapo helium, Nikel dhahabu, almasi na madini mengine yanafanyiwa tafiti katika maeneo mbalimbali, hivyo niwahakikishie watanzania Sekta ya Madini iko salama chini ya Rais Samia Suluhu,” alisema Dkt. Biteko. 

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Adolf Ndunguru alitumia fursa hiyo kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu kwa kuendelea kuiwezesha Sekta hiyo kutekeleza majukumu yake kikamilifu na kwa tija kuhakikisha malengo yaliyowekwa yanafikiwa. 

Ndunguru amesema Wizara ya Madini kupitia, Tume ya Madini inaendelea na utekelezaji wa majukumu yake kikamilifu kwa mujibu wa Sheria ya Madini Sura ya 123 ikiwemo ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali yanayotokana na shughuli za madini, kupitia utoaji na usimamizi wa leseni za madini, kusimamia na kudhibiti uchimbaji, uchakataji na biashara ya madini nchini.

“Itakumbukwa kuwa, Mwaka wa Fedha 2021/2022 Wizara ya Madini ilikusanya shilingi bilioni 623.2 sawa na asilimia 95.8 ya lengo la kukusanya shilingi bilioni 650, kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 Wizara ya Madini imewekewa lengo la kukusanya shilingi bilioni 822 sawa na wastani wa shilingi bilioni 68.5 kwa mwezi,” amesema Ndunguru. 

Aidha, Ndunguru ameongeza kuwa, katika kipindi cha mwezi Julai, 2022 Wizara ya Madini imekusanya jumla ya shilingi bilioni 57.6 sawa na asilimia 84.05 ya lengo kwa kipindi husika.

ReplyForward

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals