[Latest Updates]: Uwe mzawa uwe mwekezaji wa nje kwangu haki yako utaipata-Biteko

Tarehe : July 2, 2019, 5:31 a.m.
left

Na Issa Mtuwa -WM – Dodoma

Uwe mzawa, uwe mwekezaji wa nje kwangu haki yako utaipata. Ni kauli ya Waziri wa Madini Doto Biteko wakati akisuluhisha mgogoro baina ya wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu eneo la Ikungi mkoani Mara na mwekezaji wa kampuni ya PolyGold (T) Ltd.

Ametoa kauli hiyo leo Julai 2, 2019 ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma baada ya kukutana na pande hizo mbili  ambazo awali zilikubaliana na kusainiana mkataba wa kuchimba madini kwa ushirika. Pande hizo zilishindana kabla ya kuanza kwa shuguli za uchimbaji  kiasi cha kuwa na mgogoro mkubwa uliopelekea kufikishana kwa Waziri wa Madini ili kupata suluhu ya mgogoro wao ambao teyari umetatuliwa na Waziri Biteko.

Akitumia staili ya ushirikishi wa kusikiliza kila upande, Biteko alitoa fursa ya kila upande kuongea na kubaini changamoto kadhaa. Baada ya kuwasikiliza, Biteko alifikia maamuzi ya kuwatoa nje wawakilishi wa Kampuni ya PolyGold (T) Ltd nje ya ukumbi wa kikao ili azungumze na wachimbaji wadogo baada ya kugundua changamoto kwa upande wao.

Hali aikuwa shwari kwa muda baada ya Biteko kucharuka baada ya kubaini uwepo wa ujanja ujunja kwa upande wa wachimbaji wadogo na kuwataka waache ujanja ujanja na kusikiliza maneno ya watu walio nje na makubaliano na mshirika wao na kuwaambia waache tamaa badala yake waheshimu makubaliano waliyofikia kwa hiyari yao bila uwepo wa wizara.

Amesema yapo malalamiko ya wawekezaji katika maeneo mbalimbali ya uwekezaji hivyo hataki kuruhusu ujanja ujanja huo utokee kwenye wizara anayo iongoza. Ameongeza kuwa hata kama wao ni kutoka nje wanayo haki ya msingi kupewe haki yao pale inapoonekana kukiukwa au kuonewa kwani shuguli zao ni halali na wanafuata sheria.

“Ndugu zangu niwaambie ukweli, huyu mmoja mnae muona (Mwekezaji) ana haki kama nyinyi, akionewa huyo mjue anawatu yuma yake, ana ubalozi hapa kwa hiyo siko teyari kuchafua jina la serikali na wizara ninayo iongoza kwa kukiuka haki ya upande fulani. Uwe mzawa uwe mwekezaji wa nje kwangu haki yako utaipata, kwa hiyo kaeni na mkubaliane na mwekezaji wenu, mimi na wezangu tunatoka tunawacha nikirudi tupate majibu msimamo wangu nimewapa”. alisema Biteko huku akiwa amekasirika.

Mara baada ya maelekezo hayo wachimbaji wadogo wakiongozwa na Edwin Mchihiyo na Sosy Mgonya ambae leseni yake imenusurika kufutwa na waziri walikaa pamoja na mwekezaji wao kampuni ya PolyGold (T) Ltd iliyo wakilishwa na Sergey Sagsyan na Benny Haule na kuzungumza kuhusu mvutano juu ya mgogoro wao na kufikia muafaka uliopelekea kuondoa mgogoro uliokuwepo.

Akiongea kwa niaba ya wenzake kiongozi wa wachimbaji hao wadogo Edwin Mchihiyo amemshukuru Waziri kwa kusimamia kutatua mgogoro wao ambao umefikia tamati na kuahidi wanakwenda kutekeleza makubaliano yaliyokuwa yanaleta sinto fahau baina yao.

Katika kikao hicho Waziri aliambatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila, Mtendaji Mkuu wa Tume ya Madini Prof. Shukrani Manya, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Issa Nchasi na Mkurugenzi wa Huduma za Sheria Edwin Igenge wote kutoka wizara ya madini na viongozi wengine wa Wizara na Tume ya Madini.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals