Tarehe : June 18, 2020, 10:39 a.m.
Na Issa Mtuwa – Chamwino Dodoma
Imeelezwa kuwa, utatuzi wa migogoro ya wachimbaji wadogo wa madini hutatuliwa kwa kufuata Sheria na taratibu zinazosimamia sekta ya Madini. Utatuzi huo hufanywa pasipo ubaguzi wa hali au namna yeyote ya wahusika wanaohusishwa katika mgogoro huo.
Hayo yamebainishwa tarehe Juni 17, 2020 na Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo, alipokuwa Wilaya ya Chamwino Tarafa ya Itiso Kijiji cha Kwahemu alipotembelea kwa ajili ya kutatua mgogoro baina ya wachimbaji wadogo na Mwekezaji wa Kampuni ya Ruvu Gamstone.
Mgogoro huo umejitokeza kufuatia wachimbaji wadogo wa Kijiji cha Kwahemu wakiomba Serikali imnyang’anye mwekezaji wa Ruvu Games Stone moja ya sehemu ya leseni zake ili wapewa Umoja wa vikundi vya wachimbaji wadogo Kwahemu huku wakidai moja ya leseni wanayoitaka kutoka kwa Ruvu Gamstone inamilikiwa kihalali.
Akiwa kwenye nyakati tofauti na wachimbaji wadogo na wananchi, Nyongo aliwaeleza kuwa utatuzi wa migogoro hutatuliwa kwa kuzingatia Sheria na sio kwa ubaguzi. “Nimesikia kuwa moja ya malalamiko yenu wachimbaji kuwa Mwekezaji mnae msema sio mtanzania, niwaambie ukweli huyu ni Mtanzania na ndio aina ya leseni aliyopewa humilikiwa na Watanzania kwa mujibu wa Sheria” alisema Nyongo.
Aliongeza kuwa Kampuni ya Ruvu Gamstone leseni zake alizipata kwa uhalali na anazilipia tozo kwa mujibu wa sheria hivyo, serikali haiwezi kumnyang’anya, bali kutokana na mahitaji yenu serikali itazangumza na Mwekezaji ili kuona namna ya kupewa sehemu ya kuchimba kukidhi mahitaji yenu jambo ambalo Mwekezaji hajakataa kutoa bali kuweka utaratibu vizuri.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Umoja wa Vikundi 14 vya Wachimbaji wadogo wa Kijiji cha Kwahemu Hussein Ally Kimolo, wachimbaji hao waliomba kupatiwa moja ya leseni yenye uzalishaji (productive) ili waweze kuchimba huku wakidai sehemu walizopewa kuchimba hazina uzalishaji huku wakidai kuwa Mwekezaji huyo sio mzawa na pia eneo wanalolitaka haliendelezwi.
Akipitia mapendekezo ya utatuzi wa mgogoro huo chini ya mwenyekiti wa kamati hiyo Remidius Emmanuel Afisa Tarafa kwa niaba ya Mkuu wa wilaya, Nyongo na wajumbe waliokuwepo kwenye kamati hiyo walikubaliana kuwa mapendekezo yaaliyotolewa kwenye kamati hiyo hayakuwa makubaliano ya kamati. Mapendekezo yalikuwa binafsi na kulikuwa na mvutano baina ya wajumbe wa kamati.
Kwa upande wa Kampuni ya Ruvu Gamstone, Mkurugenzi Dimitri Mantheakis alisema, kwanza anamiliki leseni hizo kwa uhalali na kwa mujibu wa Sheria. Ameongeza kuwa suala la kutoa eneo kwa ajili ya wachimbaji haoni shida bali kuwe na utaratibu. Alisisitiza kwamba, kutoa leseni na kuwapa, wenda wakaiuza kwa Mwekezaji mwingine kama walivyo wahi uza leseni kwa Mwekazi mwingine kwa asilimia 65 japo haikuwa leseni yake.
Ameongeza kuwa hata sehemu wanayochimba ametoa yeye, na kwamba hata wakiamua yupo teyari kutoa zana za uchimbaji za kisasa, kutoa chakula ili mradi madini hayo auziwe yeye mwenye leseni kwa mujibu wa sheria kwa bei halali ya serikali.
Kufuatia mjadala huo, makundi yote kwa pamoja yalikubaliana chini ya Umwenyekiti wa Mkuu wa Wilaya kukutana Alhamisi ijayo pamoja na Afisa Madini Mkoa wa Dodoma, uongozi wa wa Wachimbaji Madini, Wanavikundi na Kampuni ya Ruvu GamStone kumalizia makubaliano ya pamoja ya utatuzi huo na taarifa kuwasilisha ripoti kwa Naibu Waziri siku ya Ijumaa.
by: madini
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…
by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…
by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.
’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…
by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…
by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.