[Latest Updates]: Zimbabwe Yapongeza Mifumo ya Utunzaji Taarifa za Madini Tanzania

Tarehe : Dec. 5, 2023, 6:58 p.m.
left

Na. Wizara ya Madini , Dodoma.

Ujumbe wa Wataalam kutoka Wizara ya Madini na Maendeleo ya Migodi  nchini Zimbabwe umeipongeza  Wizara ya Madini  kuwa na mfumo mzuri wa Usimamizi wa Leseni za Madini ujulikanao Mining Cadastre Information Management System (MCIMS) unaotumia Teknolojia  shirikishi katika utunzaji wa taarifa  za madini.
 
Hayo yamebainishwa leo Desemba 5 , 2023 jijini Dodoma  na Mkurugenzi Mkuu wa Huduma za Uendeshaji Migodi Wizara ya Madini nchini Zimbabwe Charles Simbalache wakati  mafunzo kuhusu mfumo wa  MCIMS unaotumika Tanzania.

Ikiwa siku ya kwanza ya mafunzo maalum kwa ujumbe huo, Wataalam wa Wizara ya Madini Tanzania wakiongozwa na Kamishna Msaidizi Francis Mihayo wameeleza juu ya  mfumo mzima wa MCIMS unavyofanyakazi kuanzia hatua ya awali za kujisajili huku akieleza faida zinazopatikana ndani ya mfumo huo.

Sambamba na hapo, ujumbe huo umejifunza  kuhusu Sheria za Madini na Kanuni zake, Muongozo wa Sera ya Madini, mifumo ya  utoaji leseni pamoja na aina zake .

Pia, ujumbe huo umeelezwa jinsi Wizara ya Madini inavyosimamia maendeleo ya migodi nchini na  namna ya kujikinga na majanga katika migodi na jinsi  inavyosimamia utunzaji wa mazingira maeneo yenye migodi.

Kwa upande wake, Naibu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Teknolojia ya Mawasiliano Wizara ya Madini Zimbabwe, Bi. Susane Kachote, amesema kuwa lengo la ziara hii ni kupata mafunzo kuhusu namna bora kuimarisha na kuweka teknolojia ya kuweza kusimamia mnyororo mzima wa sekta.

"Pamoja na usimamizi pia tukiwa na mifumo mizuri itasaidia kuzuia mianya ya utoroshaji madini nchini Zimbabwe" Kachote amesema

Awali, akifungua mafunzo hayo Kamishna Msaidizi kutoka Wizara ya Madini Francis Mihayo amesema kuwa Tanzania inatajwa kufanya vizuri katika sekta ya madini kutokana na kuwepo kwa mifumo mizuri ya usimamizi kuanzia ngazi ya uchimbaji mdogo mpaka mkubwa, jambo linalopelekea mataifa mengine kuja Tanzania kujifunza namna  ya usimamizi wa mifumo hiyo.

Kutokana na kufanana kwa jiolojia nchi ya Tanzania na Zimbabwe zimekuwa zikishirikiana katika kubadilishana uzoefu  katika sekta ya madini.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals