[Latest Updates]: Mavunde Aishukuru Korea Kusini Kuichangua Sekta ya Madini Tanzania

Tarehe : Sept. 3, 2023, 9:23 a.m.
left

 

Waziri wa Madini Anthony Mavunde ameishukuru Serikali ya Korea Kusini kwa kuichagua  Sekta ya Madini Tanzania kufuatia mazungumzo na kampuni kubwa za nchini humo zinazohusika  na mnyororo wa thamani wa uzalishaji betri za magari.

Mazungumzo hayo yalilenga kujadili fursa za uwekezaji zilizopo katika Sekta ya Madini nchini na kuona namna ya kushirikiana baina ya nchi hizo hususan katika kuendeleza Madini ya kimkakati.

"Tanzania inaweka kipaumbele katika uchimbaji wa Madini Mkakati kwa kufanya tafiti za madini hayo ili kuendana na soko hilo duniani. Miradi mbalimbali ya Madini Mkakati inaendelea kutekelezwa katika Sekta ya Madini ikiwemo ya Lindi Jumbo na Kabanga Nikeli", alisema Waziri Mavunde.

Viongozi wa kampuni hizo zinajumuisha kampuni za kubwa za uzalishaji magari za Posco Holdings, Posco International,SK, Korea Zinc  na LX International.
 
 Ujumbe huo  ulikutana na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Septemba 2, 2023 jijini Dar Es Salaam ambapo 
Waziri Mkuu aliuhakikishia ujumbe huo kuwa Serikali ya Tanzania ipo tayari kwa uwekezaji wao na itawawezesha kuwekeza mitaji yao. 

“Sisi tuna madini na ninyi ndugu zetu Wakorea mna mitaji, twende tuunganishe nguvu kwa manufaa ya nchi zote," alisisitiza Waziri Mkuu.


Viongozi wa kampuni hizo zinajumuisha kampuni za kubwa za uzalishaji magari za Posco Holdings, Posco International,SK, Korea Zinc  na LX International.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals