[Latest Updates]: Biteko autaka Mgodi wa Katavi na Kapufi kuajiri watanzania

Tarehe : April 28, 2018, 2:33 p.m.
left

Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko ameupa Siku 14 Mgodi wa Dhahabu wa Katavi & Kapufi uliopo Mkoani Katavi kuhakikisha uwe umepunguza wafanyakazi wa kigeni na kuajiri Watanzania kwenye nafasi wanazomudu kama Sheria inavyoelekeza.

Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (kushoto) akijadiliana jambo na Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Lilian Matinga (katikati) wakati wa kukagua shughuli ziazofanyika kwenye Mgodi wa Dhahabu wa Katavi & Kapufi Ltd uliopo Mkoani Katavi.[/caption]

Alitoa agizo hili jana Tarehe 24 Februari, 2018 alipofanya ziara kwenya mgodi huo ili kujionea shughuli zinazofanyika katika mgodi huo.

Taarifa ya mgodi iliyowasilishwa kwake ilibainisha kuwa jumla ya wageni 48 wameajiriwa na huku 36 kati yao wakiwa hawana ujuzi na wanafanya shughuli ambazo Watanzania wanamudu, ikiwemo ya ulinzi.

Biteko alisema dhamira ya Serikali ni kuona Watanzania wananufaika na Sekta ya Madini kwa namna mbalimbali ikiwemo ya kujipatia ajira kwenye migodi na kwamba suala hilo la kuajiri wageni kwenye nafasi wanazomudu Watanzania halivumiliki.

Alimuagiza Mkuu wa Wilaya na Afisa Madini kuhakikisha wanalifuatilia jambo hilo na liwe limemalizika baada ya wiki mbili kuanzia Tarehe 24 Februari, 2018 na apatiwe mrejesho wake.

“Mnawafanyakazi wengi ambao wanafanya kazi ambazo Watanzania wanaziweza. Hatuwabagui lakini tunataka manufaa ya madini yabaki kwa Watanzania,” alisema Biteko.

Biteko aliiagiza Idara ya Uhamiaji Nchini kufuatilia Wafanyakazi wakigeni waliopo migodini ili kukagua kama wanavyo vibali vya kufanya kazi hapa nchini. “Mnavyotoa vibali muwe makini, ili shughuli zinazokuja kufanywa na wageni ziwe kweli Watanzania hawazimudu,” alisisitiza.

Alihimiza migodi yote nchini kuepuka kuwanyanyasa wafanyakazi sambamba na kuwataka wafanyakazi waliaoajiriwa migodini kufanya kazi kwa uaminifu ili kulijengea Taifa heshima inayokubalika.

Imeandaliwa na:

Mohamed Saif,

Afisa Habari,

Wizara ya Madini,

5 Barabara ya Samora Machel,

S.L.P 2000,

11474 Dar es Salaam,

Simu: +255-22-2121606/7, Nukushi: +255-22-2121606,

Barua Pepe: info@madini.go.tz,                                                                               

Tovuti: madini.go.tz

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals