Tarehe : Dec. 5, 2023, 6:55 p.m.
Dodoma.
Ujumbe wa Wataalam kutoka Taasisi ya Uhamasishaji, Uwazi, na Uwajibikaji katika Rasilimali Madini, Mafuta na Gesi Asilia nchini Ghana (GHEITI) umeipongeza, Taasisi ya Uhamasishaji, Uwazi na Uwajibikaji katika Sekta ya Madini, Mafuta na Gesi Asilia (TEITI) kwa kuzifungamanisha sekta hizo na sekta za kikodi na mazingira katika Uziduaji.
Pongezi hizo zimetolewa leo Desemba 5 , 2023 na Dkt. Steve Manteaw katika mafunzo ya kujengeana uwezo yanayoendeshwa na taasisi ya TEITI kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali za kitaalam ikiwemo Mamlaka ya Ukusanyaji Kodi Tanzania (TRA), Baraza la Taifa la Usimamizi Mazingira (NEMC), Tume ya Madini na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO).
Akizungumza mapema baada ya majadiliano ya kina na wataalam kutoka TRA Dkt. Manteaw amesema kuwa kupitia mada tunapata fursa ya kujifunza mambo mengi ya kitaalam yanayohusiana na sekta husika ambazo ni Mafuta, Madini na Gesi Asilia, hivyo tunaamini katika majadiliano pia wenzetu mnajifunza kitu kwetu hasa katika sekta ya Madini hususani Madini ya Metali.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa TEITI Tanzania CPA. Ludovick Utoah ameeleza kuwa Tanzania na Ghana ni nchi wanachama wa muda mrefu katika jumuhiya ya EITI, kupitia umoja huo nchi zote mbili zimejifunza jinsi ya kuweka misingi bora na iliyosalama katika mfumo mzima wa Uziduaji ikiwa pamoja na kufuata taratibu zilizowekwa na EITI katika utunzaji wa mazingira kwenye uziduaji kama mikataba tuliyosaini inavyotuelekeza.
Sambamba na kuwasilishwa kwa mada juu ya mifumo ya kifedha na ulipaji wa kodi katika Uwazi na Uwajibikaji kwenye Uziduaji pia wataalam hao wamepata fursa ya kujionea Maabara ya Uchunguzi na Utambuzi wa Madini iliyopo katika Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) na kutembelea makumbusho ya Taifa ya Madini na Miamba. Umoja wa Kimataifa EITI una jumla ya nchi wanachama (57), Ghana ikiwa nchi mwanachama tangu mwaka 2003 hadi sasa GHEITI imeshatoa ripoti (14) za ulinganishi wa malipo ya kodi na mapato kutoka katika sekta ya uziduaji. https:
by: madini
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…
by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…
by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.
’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…
by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…
by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.