[Latest Updates]: Serikali yaitaka Stamigold ijiendeshe kibiashara

Tarehe : March 28, 2018, 10:49 a.m.
left

  • Katibu Mkuu Madini atoa siku 14 kwa uongozi kuwasilisha mpango mkakati

Serikali imetoa siku 14 kwa kampuni ya Stamigold, inayomiliki Mgodi wa Dhahabu uliopo Biharamulo mkoani Kagera, kuandaa mpango mkakati wa kibiashara, utakaobainisha namna itakavyojiendesha pasipo kuitegemea Serikali.

Wafanyakazi mbalimbali wa Kampuni ya Stamigold wakitoa maoni yao kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila (hayupo pichani) alipowatembelea hivi karibuni.[/caption]

Agizo hilo lilitolewa jana, Januari 6, 2018 na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila alipotembelea Mgodi huo na kuzungumza na Menejimenti pamoja na wafanyakazi wake.

Profesa Msanjila alisema kuwa lengo la Serikali kupitia Wizara ya Madini, ni kuona Kampuni tanzu hiyo ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), inajiendesha kibiashara na kiushindani ili ipate faida stahiki na kulinufaisha Taifa kama ilivyo dhamira ya kuanzishwa kwake, na siyo vinginevyo.

“Menejimenti ya Kampuni, Bodi pamoja na Menejimenti ya STAMICO, nawapa hadi tarehe 21 mwezi huu, kila upande uwe umewasilisha mapendekezo ya kimkakati yanayobainisha namna gani Stamigold itaweza kusimama yenyewe na kujiendesha kiushindani kama zilivyo kampuni nyingine za kibiashara. Kwa upande wetu, Kamishna wa Madini na mimi Katibu Mkuu pia tutakuja na mapendekezo yetu.”

Akifafanua zaidi, Katibu Mkuu alisema Serikali imewekeza kwa kiasi kikubwa katika kampuni ya Stamigold hivyo haitakubali kuona mgodi huo unaendeshwa kwa hasara. “Kila mtu awajibike kwenye eneo lake,” alisisitiza.

Alisema, pamoja na kuwa Stamigold ni kampuni ya Serikali lakini imesajiliwa na Taasisi inayotoa leseni za biashara ya Brela, hivyo inapaswa kujiendesha kama kampuni nyingine za kibiashara. “Kampuni ya serikali ambayo haifanyi biashara haiendi kujiandikisha Brela. Ninyi mnafanya biashara hivyo lazima mfanye kazi kibiashara.”

Aidha, Profesa Msanjila aliutaka uongozi wa kampuni kuhakikisha unaweka wazi taarifa zote za mapato na matumizi kwa wafanyakazi wote ili waelewe wanazalisha kiasi gani, wanapata faida kiasi gani, matumizi ni kiasi gani na kama kuna hasara ibainishwe wazi.

Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Stamigold, wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila (hayupo pichani), alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara yake hivi karibuni.[/caption]

Alifafanua kuwa utaratibu wa kuweka wazi mapato na matumizi kwa wafanyakazi wote utaondoa manung’uniko kwani utaratibu wa kibiashara unamtaka mwajiri amlipe mfanyakazi kulingana na mapato. “Huwezi kumlipa mtu mshahara hata pale ambapo hazalishi. Hii siyo sawa kibiashara maana lazima utapata hasara. Huu ndiyo ukweli ndugu zangu. Tubadilike. Hakuna hela ya kuchezea.”

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Mhandisi John Nayopa alimhakikishia Katibu Mkuu kuwa maagizo yote aliyoyatoa yatatekelezwa ndani ya muda alioelekeza. Aidha, aliwataka wafanyakazi wa Stamigold kutoa ushirikiano kwa kutoa maoni na ushauri wao wakati wa kuandaa mpango mkakati huo utakaoiwezesha Kampuni kujiendesha kibiashara.

Katika ziara hiyo, Katibu Mkuu aliambatana na viongozi wengine wa Wizara akiwemo Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimaliwatu, Miriam Mbaga, Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Ziwa Viktoria Magharibi, Mhandisi Yahaya Samamba, Kaimu Afisa Madini wa Mkoa wa Kagera, Paschal Bundala na Mhandisi Migodi kutoka wizarani, Kungulu Kasongi.

Imeandaliwa na:

Veronica Simba, Biharamulo

Afisa Habari,

Wizara ya Madini,

5 Barabara ya Samora Machel,

S.L.P 2000,

11474 Dar es Salaam,

Simu: +255-22-2121606/7, Nukushi: +255-22-2121606,

Barua Pepe: info@madini.go.tz,                                                                               

Tovuti: madini.go.tz

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals