[Latest Updates]: Utafiti Waonesha Asilimia 86.2 ya Wanawake Wanajihusisha na Shughuli za Madini

Tarehe : Aug. 27, 2024, 3:34 p.m.
left

• Wanawake 17 sawa na asilimia 1.7 wanamiliki Migodi

• Wanawake 67 sawa na asilimia 6.8  wanamiliki maeneo ya uchimbaji

• Wanawake 855 sawa na asilimia 86.2 wanajihusisha na kazi zinazohusiana na uchimbaji na uchenjuaji madini

• Wanawake 53 sawa na asilimia 5.3 wanatoa huduma maeneo ya uchimbaji

Dodoma

Matokeo ya utafiti mdogo uliofanywa na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kwa kushirikiana na Chama cha Wachimbaji Wanawake Tanzania (TAWOMA) umeonesha zaidi ya asilimia 80 ya wanawake kutoka  mikoa ya Shinyanga, Geita, Mara na Simiyu wanajishughulisha na Shughuli za sekta ya Madini nchini.

Hayo yamesemwa leo Agosti 27, 2024 na Naibu Waziri wa Madini  Dkt. Steven Kiruswa alipokuwa akijibu swali lililoulizwa na Mbunge wa Viti maalumu vya wanawake Fatma Hassan aliyetaka kujua idadi ya  wanawake wanaomiliki migodi ya madini nchini.

Naibu Waziri amesema kuwa,  shughuli za madini nchini zinafanyika katika maeneo mbalimbali  kupitia watu binafsi na kampuni ambazo ndani yake kuna wanawake na wanaume.

Ameongeza kuwa, utafiti uliohusisha wanawake 992 umeonesha Wanawake 17 sawa na asilimia 1.7 wanamiliki migodi, wanawake 67 sawa na asilimia 6.8 wanamiliki maeneo ya uchimbaji (maduara) katika leseni za uchimbaji madini na wanawake 855 sawa na asilimia 8.2 wanajishughulisha na kazi zinazohusiana na uchimbaji pamoja na uchenjuaji madini huku wanawake 53 sawa na asilimia 5.3 wanatoa huduma maeneo ya uchimbaji.

Dkt. Kiruswa ameongeza kuwa  kulingana na umuhimu na mchango wanaotoa kwa taifa,  Serikali itaendelea kuwasimamia na kuwapatia leseni wanawake wanaojishughulisha na uchimbaji wa madini ili kuongeza mchango wao kwenye sekta pia kuimarisha uchumi wao.

Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 ilibaini kuwa  kuna takribani wanawake milioni 3 wanaoshiriki katika mnyororo mzima wa thamani madini. 


#InvestInTanzaniaMiningSector

#Vision2030: MadininiMaisha&Utajiri

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals