[Latest Updates]: Viongozi Madini Washiriki Warsha ya Utambuzi wa Madini

Tarehe : May 25, 2023, 12:36 p.m.
left

Viongozi Madini Washiriki Warsha ya Utambuzi wa Madini

Dar Es Salaam

Viongozi kutoka Wizara ya Madini pamoja na Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania ( GST) leo tarehe 24 Mei 2023, wamekuwa miongoni mwa wataalam wanaoshiriki katika warsha ya Siku mbili ya Utambuzi wa Asili ya Madini (Analitical Fingerprint).

Masuala ya utambuzi wa asili ya madini yanasaidia kufahamu uasili wa madini ya metali kutoka mgodi na nchi yanakochimbwa ikiwa ni mojawapo ya mikakati ya udhibiti biashara haramu ya madini.

Warsha hiyo inayofanyika katika Hotel ya Bahari Beach jijini Dar Es Salaam imeandaliwa na Jumuiya ya Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu (ICGLR) na Shirika la Maendeleo la Ujerumani (BGR).

Mbali na washiriki kutoka Tanzania, washiriki wengine wanatoka katika nchi za Burundi, DRC, Rwanda na Uganda. Aidha, Sekretariati ya ICGLR kutoka nchini Burundi, mwakilishi kutoka African Minerals and Geosciences Centre (AMGC) na wawakilishi kutoka BGR wanashiriki warsha hiyo.

Katika warsha hiyo, Wizara imewakilishwa na Mtendaji Mkuu wa GST, Dkt. Mussa Budeba, Mkaguzi Mkuu wa Ndani kutoka Wizara ya Madini Bw. Mathias Abisai na Mkurugenzi wa Huduma za Jiolojia kutoka GST Dkt. Ronald Massawe.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals