[Latest Updates]: Mchango wa Mapato Yatokanayo na Masoko ya Madini Waongezeka

Tarehe : Sept. 8, 2022, 7:59 a.m.
left

STAMICO kufungua ofisi ya ununuzi wa dhahabu Kongo

Imeelezwa kuwa, mchango wa mapato yatokanayo na masoko ya madini yameongezeka kutoka asilimia 2.62 toka kuanzishwa kwake hadi kufikia asilimia 28.36 katika Mwaka wa Fedha 2021/22.

Msingi wa uanzishwaji wa Masoko ya Madini ni kupata takwimu sahihi za mauzo ya madini, kuwasadia wachimbaji wadogo kupata soko la uhakika, kupata bei stahiki kwa bidhaa za madini pamoja na kudhibiti utoroshaji wa madini nchini.

Hayo yamebainishwa na Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini Mhandisi Yahya Samamba wakati akiwasilisha taarifa kuhusu hali ya uendeshaji wa masoko ya madini nchini kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini jijini Dodoma.

Samamba amesema, uanzishwaji wa Masoko ulianza rasmi Machi, 2019 ambapo hadi kufikia mwezi Julai, 2022 yameanzishwa masoko ya madini 42 na vituo vya ununuzi wa madini 78 nchini.

Sambamba amesema usimamizi wa masoko nchini umeendelea kuimarika ambapo mpaka Julai, 2022 kiasi cha kilogramu 51,539.61 za dhahabu, karati 58,747.78 za almasi, kilogramu 606,253.82 za madini ya bati, kilogramu 284,670.66 na karati 344,370.28 za tanzanite pamoja na kilogramu 10,985.79 na karati 65,033.72 za madini mbalimbali ya vito yaliuzwa kupitia masoko hayo na kuipatia Serikali jumla ya shilingi bilioni 422.32.

Aidha, Samamba amesema katika kipindi cha Mwaka wa Fedha 2021/22 masoko ya madini yamechangia kiasi cha shilingi bilioni 264.09 sawa na asilimia 28.36 ya mapato yatokanayo na shughuli za madini.

Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Dkt. Vanance Mwasse amewasilisha taarifa kuhusu hali ya Kiwanda cha kusafisha dhahabu cha Mwanza Precious Metal Refinery Ltd kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini.

Dkt. Mwasse amesema kiwanda hicho cha kusafisha dhahabu ni cha kwanza kujengwa nchini chenye umiliki wa Serikali ndani yake ambapo kitaongeza mapato ya nchi, ajira na kitaitambulisha Tanzania kimataifa.

Pamoja na mambo mengine, Dkt. Mwasse amesema kiwanda kina mkakati wa kukamilisha mazungumzo na nchi ya Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo (DRC) kwa lengo la kupata chanzo kingine cha dhahabu ghafi na pia, kiwanda kina mpango wa kufungua ofisi ya kukusanya dhahabu katika mji wa Bukavu.

Kwa upande wake Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko ameishukuru Kamati hiyo kwa ushauri na maelekezo yake inayoyatoa mara kwa mara ambayo yamepelekea kuongeza mchango wa Sekta ya Madini katika Pato la Taifa.

ReplyForward

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals