[Latest Updates]: Waziri Biteko Awasimamisha Kazi Maafisa Madini Ofisi ya Madini Chunya

Tarehe : April 2, 2019, 4:17 p.m.
left

Na Tito Mselem, Chunya

Waziri wa Madini Doto Biteko amewasimamisha kazi Maafisa Madini wote wa Ofisi ya Madini Chunya Mkoani Mbeya na kuteua Wajiolojia watakaokaimu nafasi hizo wakati wizara ikitafuta Maafisa wengine waaminifu watakaofanya kazi hizo.

Hatua hiyo imekuja baada ya kugundua wizi mkubwa wa madini ya dhahabu unaofanywa na maafisa hao wakishilikiana na wamiliki wa kampuni ya uchenjuaji wa dhahabu.

Akizungumza katika mkutano na wachimbaji wadogo wadogo pamoja na wamiliki wa makampuni ya uchenjuaji wa dhahabu Waziri Biteko, amesema udanganyifu unaofanywa na Maafisa hao wa Madini pamoja wenye  kampuni hizo za uchenjuaji ni mkubwa na  hahuitaji msamaha hata kidogo.

“Mimi kama Waziri mwenye dhamana katika sekta hii ya Madini ninawapenda sana wachimbaji ila nasikitika sana kwa wachimbaji na wenye makampuni ya uchenjuaji kutokuwa waaminifu,” amesisitiza Waziri Biteko

Ameongeza kuwa, Maafisa wa madini hao ndiyo wanaotoa mianya ya wizi wa dhahabu unaofanyika kwenye kampuni zaa uchenjuaji wa dhahabu  wilayani humo.

Aidha, katika ziara hiyo Biteko ameifunga kampuni ya Ntorah Gold Company Ltd inayohusika na uchenjuaji wa dhahabu wilayani  humo baada ya kutoa taarifa za udanganyifu kwa serikali.

Pia, Waziri Biteko ameongeza kwamba, Wilaya ya  Chunya ndiyo sehemu pekee Tanzania inayoongoza kwa wizi wa dhahabu na kutoa taarifa za uongo za kampuni za uchenjuaji wa dhahabu ikifuatiwa na wilaya ya Kahama iliyopo Mkoani Shinyanga.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjla, amesema serikali imeondoa kodi zote kwa wachimbaji wadogo zilizokuwa zikilalamikiwa na wachimbaji pamoja na kampuni za uchenjuaji wa dhahabu lakini bado wizi unafanyika tena kwa kiwango kikubwa.  

Naye, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila amikiri kwamba hana elimu ya madini hivyo imekuwa vigumu kwake kudhibiti wizi huo   lakini anaamini wizi na udanganyifu upo tena kwa kiwango kikubwa.

“kiukweli sina elimu ya madini hasa kwenye upande wa uchenjuaji wa dhahabu, naamini kuna wizi mkubwa wa madini haya ya dhahabu na taarifa zisizo na ukweli” amesema  Chalamila.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals