[Latest Updates]: Serikali Kukamilisha Tafiti za Madini Nchini

Tarehe : Sept. 24, 2023, 9:09 a.m.
left

 

• Mpaka sasa utafiti wa kina wa jiofizikia kwa kutumia ndege umefanyika kwa asilimia 16

Serikali kupitia Wizara ya Madini ipo katika mpango wa kukamilisha utafiti wa kina wa  jiofizikia kwa kutumia ndege  kupitia Taasisi ya  Jiolojia na Utafiti wa Madini (GST).

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde  wakati akihutubia wananchi siku ya ufunguzi rasmi wa maonesho ya Teknolojia ya Madini mkoani Geita.

Akizungumza juu ya maendeleo ya Sekta ya Madini Mhe.Mavunde alifafanua kuwa Wizara kupitia Dira yake mpya ya 2030 inayosema Madini ni Maisha na Utajiri,  imeona  katika kuchochea ukuaji wa Sekta ya Madini na kuongeza mchango katika Pato la Taifa, kuna haja ya kupata taarifa za miamba na madini kwa eneo lote la nchi yetu.

Alifafanua kuwa katika kutekeleza dira hiyo pamoja na mambo mengine, Serikali itakamilisha utafiti wa kina wa jiofizikia kwa kutumia ndege  kwa asilimia 100 kutoka asilimia 16 zilizopo kwa sasa ifikapo 2030. Lengo la utafiti huo likiwa ni kuchochea zaidi uwekezaji katika Sekta ya Madini pamoja na kufungamanisha sekta ya madini na sekta  nyingine za kiuchumi.

Maonesho ya Sita ya kimataifa ya Teknolojia ya madini yalifunguliwa rasmi Septemba 23 na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko na  yatafungwa Septemba  30, 2023.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals