[Latest Updates]: FEMATA Yaishukuru Serikali kwa Mazingira Bora ya Uchimbaji Mdogo

Tarehe : July 9, 2024, 9:59 p.m.
left

Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Wadogo wa Madini Tanzania (FEMATA) limeishukuru Serikali kwa juhudi zake za kuwatengenezea mazingira bora yenye kuleta tija zaidi katika shughuli za uchimbaji mdogo na masoko ya uhakika. 

Hayo yameelezwa leo Julai 9, 2024 na Rais wa FEMATA John Bina alipotembelea banda la Wizara ya Madini na Taasisi zake katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF) maarufu kama Sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam. 

Amesema kwamba hatua ambazo zimekuwa zikichukuliwa na Serikali kupitia Wizara ya Madini zimeleta mabadiliko makubwa katika sekta ya madini nchini sambamba na kuleta tija kubwa kwa kundi la Wachimbaji Wadogo. 

Ametaja mafanikio yaliyopatikana kuwa ni pamoja na kuongezeka kwa Leseni ambapo Serikali imeongeza idadi ya leseni za uchimbaji madini kwa wachimbaji wadogo na hivyo kurahisisha shughuli zao sambamba na Usimamizi mzuri wa Masoko ya Madini na vituo vya kununulia madini ambayo imewasaidia kupata soko la uhakika kwa bei ya soko la dunia na kuongeza uwazi na kudhibiti utoroshwaji wa madini.

Bina ameongeza kuwa, Wizara ya Madini na STAMICO kwa kushirikiana na taasisi za kifedha, zimewezesha wachimbaji wadogo kupata mikopo yenye riba nafuu ili kuboresha vifaa na teknolojia wanayotumia pamoja na kukuza mitaji yao.

Vile vile, amesema kuwa  Serikali kupitia STAMICO imewapatia Wachimbaji hao mashine za uchorongaji ambazo zinawasaidia kurahisisha shughuli zao sambamba na kuongeza ufanisi na kuokoa gharama kubwa waliyokuwa wakitumia hapo awali katika uzalishaji. 

Bina ambaye ameambatana na Viongozi wa FEMATA ameongeza kuwa juhudi hizo za Serikali zimechangia kwa kiasi kikubwa katika kuboresha maisha ya wachimbaji wadogo na kuchangia ukuaji wa sekta na hatimaye mchango wao katika Pato la Taifa. 

Pia, Rais huyo wa FEMATA ameiomba Serikali na wadau wa sekta ya madini kuendelea na juhudi hizo na kuahidi ushirikiano wao wa dhati ili kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu katika sekta ya madini nchini Tanzania.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals