[Latest Updates]: Dkt. Kiruswa aumaliza mgogoro wa Wachimbaji Madini Handeni

Tarehe : June 23, 2023, 10:20 a.m.
left

Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa ameufungua Mgodi wa wachimbaji wadogo wa Madini ya Dhahabu uliofungwa baada ya kuumaliza mgogoro kati ya wachimbaji wadogo wa Madini ya Dhahabu na mmiliki wa leseni ya uchimbaji mdogo Godfrey Bitesigirwe katika eneo la Kwandege Kijiji cha Mlimamzinga wilaya ya Handeni Mkoani Tanga.

Dkt. Kiruswa ameufungua mgodi huo baada ya kumaliza mgogoro uliodumu kwa muda mrefu kati ya wachimbaji hao na mmiliki wa leseni hiyo wilayani humo  baada ya kutembelea eneo la machimbo hayo na kuzungumza na wachimbaji wadogo wa madini katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la mgodi huo.

Aidha, Dkt. Kiruswa amewataka wachimbaji wadogo kufanya shughuli za uchimbaji wa madini katika eneo hilo kwa siku 90 kama alivyoagiza Mkuu wa Wilaya hiyo kabla ya kuufunga Mgodi huo na kumtaka mImiliki wa leseni hiyo kutoa ajira kwa wachimbaji wadogo wanaotarajiwa kupisha eneo la leseni hiyo ili rasilimali hiyo iweze kuwafaidisha wote.

Pamoja na mambo mengine, Dkt. Kiruswa ametoa anyo kwa wachimbaji wadogo na wafanyabishara wa madini wanaotorosha madini kwa lengo la kukwepa kodi ya Serikali ambapo amewataka kufuata Sheria na Kanuni zilizowekwa na Serikali ikiwemo kuuza madini katika Masoko na Vituo vya Ununuzi wa Madini.

Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Handeni Vijijini John Sallu amempongeza Dkt. Kiruswa kwa kuumaliza mgogoro uliokuwepo katika eneo hilo ili wachimbaji hao wachimbe kwa tija na wanufaike  na rasilimali madini katika wilaya hiyo .

Pia, Sallu ameiomba Wizara ya Madini kutenga maeneo  kwa ajili ya wachimbaji wadogo hususan maeneo yenye leseni ya utafiti yaliyoisha muda wake ili waweze kufaidika na rasilimali madini zilizopo wilayani humo.


Awali, Dkt. Kiruswa alitembelea Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Handeni kwa lengo la kupata taarifa ya shughuli za uchimbaji na uchenjuaji wa madini zilizopo wilayani humo.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals