Tarehe : Dec. 28, 2017, 9:25 a.m.
Serikali imesema inaangalia namna ya kuwasaidia wachimbaji Wadogo wa Madini ili kuwa na uchimbaji wenye manufaa kwao na Taifa kwa ujumla.
Wananchi na Wachimbaji Wadogo wa maeneo yanayozunguka uliokuwa mgodi wa Resolute wa Nzega wakimsikiliza Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (hayupo pichani).[/caption]
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo alisema hayo Desemba 15, 20017 alipotembelea eneo lililokuwa Mgodi wa Resolute Wilayani Nzega Mkoani Tabora.
Nyongo alisema kuwa Serikali imebaini kwamba uchimbaji Mdogo wa Madini hauleti tija kwa wachimbaji wenyewe na kwa Serikali hasa ikizingatiwa kuwa mapato yatokanayo na uchimbaji siyo ya kuridhisha kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ukosefu wa elimu, taarifa sahihi na vifaa kwa wachimbaji.
“Tumegundua wachimbaji wadogo walio wengi wanahitaji msaada mkubwa kutoka serikalini ili wawe na uchimbaji wenye tija, si kwao tu bali kwa Taifa kwa ujumla,” alisema.
Akizungumzia Mgodi wa Resolute ambao ulisitisha uchimbaji madini tangu Mwaka 2014, Nyongo alisema wapo wachimbaji wadogo ambao wamekuwa wakivamia na kufanya shughuli za uchimbaji kwenye mashimo hayo jambo ambalo alisema linahatarisha maisha yao.
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo akizungumza na wananchi na wachimbaji wadogo katika Kijiji cha Nhobola wilayani Nzega Mkoani Tabora (hawapo pichani).[/caption]
Alionya wavamizi wa maeneo hayo kuacha mara moja, kwani kuendeleza shughuli za uchimbaji kwenye mashimo yaliyoachwa na Resolute ni kuhatarisha uhai. “Nimetembelea na nimeona mashimo mengi ambayo yamechimbwa na wachimbaji wadogo lakini bahati mbaya hayajazingatia utaratibu wa uchimbaji,” alisema.
Aliongeza kuwa, Mwaka 2016 watu wapatao Sita walifariki baada ya kudondokewa na mwamba wa mawe kwenye mgodi huo wa Resolute eneo ambalo lilipigwa marufuku ya uchimbaji kutokana na hatari iliyopo ya kuangukiwa na vifusi.
Aliwaasa wachimbaji hao kuwa na subira kwani dhamira ya Serikali ni kuwasaidia kuwa na uchimbaji utakaowaletea manufaa zaidi kuliko namna hiyo ya uchimbaji wanayoifanya hivi sasa ikiwemo kuwapatia maeneo mazuri na salama yaliyofanyiwa utafiti na elimu ya uchimbaji sahihi.
Alimuagiza Afisa Madini Mkazi Tabora, Laurent Mayala kushirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Nzega kuhakikisha wanatembelea eneo hilo mara kwa mara ili kuepusha maafa.
Imeandaliwa na:
Mohamed Saif,
Afisa Habari,
Wizara ya Madini,
5 Barabara ya Samora Machel,
S.L.P 2000,
11474 Dar es Salaam,
Simu: +255-22-2121606/7, Nukushi: +255-22-2121606,
Barua Pepe: info@madini.go.tz,
Tovuti: madini.go.tz
by: madini
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…
by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…
by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.
’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…
by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…
by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.