Tarehe : Oct. 19, 2024, 1:01 p.m.
Awahamasisha Watumishi kujiandikisha kwenye daftari la Wapiga Kura Serikali za Mitaa
GST Yazoa Medali za kutosha
Madini Yanga Yanyakua Ubingwa
Dodoma
Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde ameeleza kuhusu umuhimu wa Madini Bonanza na kueleza kuwa limelenga kuimarisha umoja, mshikamano na ushirikiano baina ya Watumishi wa Wizara na Taasisi zake ili kuifanya Wizara kuwa familia moja.
Amesema hayo leo Oktoba 19, 2024 katika Viwanja vya Shule ya Sekondari John Merlin – Miyuji jijini Dodoma, wakati akizungumza katika Madini Bonanza lililowajumuisha Watumishi wa Wizara ya Madini na Taasisi zake.
" Ninawapongeza kwa bonanza hili kwasababu linatusaidia kukaa pamoja, kufurahi na kufahamiana zaidi," amesema.
Aidha, amewasisitiza watumishi kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi ili kuimarisha afya zao, na kuongeza," kama mnavyofahamu hivi sasa takwimu zinaonesha kuna changamoto kubwa ya magonjwa yasiyoambukiza hivyo kuna umuhimu mkubwa wa kufanya mazoezi,".
Katika hatua nyingine, Mhe. Mavunde amewahamasisha watumishi wa Wizara kujishiriki katika zoezi linaloendelea hivi sasa la kujiandikisha kwa ajili ya uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mitaa unaotarajia kufanyika mwezi Novemba mwaka huu.
Kwa upande wake, Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Madini Terence Ngole ameeleza kuhusu mashindano ya michezo mbalimbali yaliyofanyika yakihusisha mpira ya miguu, pete, kamba, mbio za mita 100 na mita 400 ambapo washindi mbalimbali wamepatikana kutoka Wizara na Taasisi zake huku Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania ( GST) ikiondoka na medali lukuki na makombe.
#MichezoniAfya
#MichezoniFuraha
#MichezoniAjira
#Vision2030: MadininiMaishanaUtakiri
by: madini
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…
by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…
by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.
’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…
by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…
by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.