Tarehe : Aug. 18, 2024, 4:11 p.m.
●Eneo la Lemishuko kurushwa ndege nyuki ya Utafiti
●Serikali kutatua changamoto ya Maji,Umeme,Barabara na Zahanati
●Aongoza Harambee ya ujenzi wa Zahanati Lemishuku_
●Jengo la Kituo cha ununuzi wa Madini kukamilika Desemba,2024_
●Wachimbaji wamshukuru Rais Samia kwa kufungua sekta ya madini_
SIMANJIRO,MANYARA
WAZIRI wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde amefanya ziara kukagua shughuli za uchimbaji madini na kusikiliza changamoto za wachimbaji wadogo katika eneo la Lemishuku,Wilayani Simanjiro eneo ambalo ni maarufu kwa uchimbaji wa madini vito ya Green Garnet
Waziri Mavunde amepata nafasi ya kukagua uwekezaji uliofanywa katika uchimbaji wa madini katika Kijiji cha Lemishuku na kuahidi kwamba Serikali itafanikisha urushwaji wa ndege nyuki “drone” katika eneo hilo kwa ajili ya utafiti wa kina ili kuwaongoza vizuri wachimbaji wadogo kuondokana na uchimbaji wa kubahatisha na kuongeza kuwa mwishoni mwa mwezi Desemba 2024 jengo la kituo cha ununuzi wa Madini litakuwa limekamilika ili kufanikisha urahisi wa Biashara ya madini.
Aidha,Waziri Mavunde alieleza kuwa Serikali ya awamu ya sita chini ya Mh. Rais Dkt. Samia S. Hassan itatatuwa Changamoto zote za Maji,Umeme,Barabara na Zahanati ili kuchochea shughuli za ukuaji wa sekta ya madini ambapo katika ujenzi zahanati aliongoza harambee ambayo jumla ya matofali 4500,sarufi mifuko 183 na fedha Tsh 23m zimepatikana.
Akitoa salamu zake Mbunge wa Simanjiro, Mh. Christopher Ole Sendeka, amemshukuru Mh. Rais Dkt. Samia S. Hassan kwa kazi kubwa ya kuboresha huduma za kijamii katika eneo hilo la uchimbaji na kumshukuru Waziri Mavunde kwa kuwa Waziri wa kwanza kufika katika eneo hilo kusikiliza na kutatua kero za wachimbaji.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Wadogo (FEMATA) John Bina na Mwenyekiti wa Mabroka Tanzania (CHAMATA) Ndg. Jeremiah Kituyo wameipongeza serikali kupitia wizara ya madini kwa mipango ya uendelezaji wa sekta ya madini na kusisitiza kwa wachimbaji wadogo kuzingatia sheria za nchi na pia kwa wafanyabiashara wa madini kuhakikisha wanakata Leseni ya biashara ya madini ili kuepuka usumbufu usio wa lazima.
Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro,Mh. Fakhi Lulandala amewahakikishia wachimbaji wadogo wa eneo la Lemishuku kwamba Serikali ya ngazi ya Wilaya kupitia Taasisi mbalimbali zilizopo hapo zitahakikisha zinasimamia kwa ukaribu utekelezaji wa changamoto za wachimbaji ili kuweka mazingira mazuri ya uchimbaji katika eneo la Lemishuku.
by: madini
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…
by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…
by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.
’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…
by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…
by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.