[Latest Updates]: TGC Yaja na Mpango wa Kutengeneza Mabilionea Kupitia Uongezaji Thamani Madini

Tarehe : Nov. 10, 2023, 7:43 p.m.
left

Kituo cha Jemolijia Tanzania (TGC) kimedhamiria kuhuisha mitaala ya mafunzo yake ili kutengeneza Watanzania matajiri  kupitia tasnia ya Uongezaji Thamani Madini.

Hayo yameelezwa leo Novemba 10, 2023, jijini Dodoma na Kaimu Mratibu wa Kituo cha Jemolijia Tanzania (TGC), Jumanne Shimba, wakati akizungumza katika kipindi cha runinga na radio cha Good Morning kinachorushwa na Wasafi Media.

Amesema kuwa katika kuhakikisha TGC inaendana na Vision 2030, Madini ni Maisha na Utajiri, kituo hicho kimekuja na mkakati wa kuhuisha mitaala yake ili kutengeneza vijana na wanawake wengi kupitia mafunzo ya usonara kwa lengo la kuongeza thamani madini na kunufaika sio kwa kuchimba tu madini hapa nchini bali kuchonga, kuremba na kung’arisha mapambo kutoka kwenye miamba tofauti ya madini.

Ameongeza kuwa, TGC ina mkakati wa kuanzisha maabara ya Madini ya Vito itakayopatikana katika jengo jipya la taasisi hiyo litakalojengwa jijini Arusha sambamba na viwanda vya kuchakata na kuongeza thamani madini ya vito yanayopatikana nchini kwa kwamba kwa kufanya hivyo itaongeza mchango wa madini hayo katika pato la taifa tofauti na yakisafirishwa nje ya nchi na kwenda kuongezewa thamani katika nchi nyingine.

Amewahimiza watanzania kujijengea hulka ya kununua urembo na mapambo yanayotokana na madini hayo yanayoongezewa thamani hapa nchini ili kusaidia vijana na wanawake wa kitanzania wanaofanya shughuli hizo kupata soko la uhakika lakini pia kutangaza bidhaa za kitanzania ndani na nje ya mipaka.

Aidha, ametoa wito kwa Watanzania kujitokeza kwa wingi kujiunga na kituo hicho ili kujifunza mbinu za uongezaji thamani madini na kupata uwezo wa kujiajiri wenyewe kupitia taaluma hiyo hivyo kujipatia vipato sambamba kujiinua kiuchumi kuanzia ngazi ya familia hadi taifa kwa ujumla kupitia mnyororo wa uongezaji thamani madini.

Kituo cha Jemolijia Tanzania (TGC) kinapatikana jijini Arusha na kilianzishwa mwaka 2003, kwa lengo la kutoa mafunzo ya ndani kuhusu uchongaji miamba na madini ya vito kwa nia ya kuongeza ujuzi wa kuongeza thamani. Hivi sasa kituo hicho kinatoa mafunzo kwa ngazi ya Stashahada na Astashada kikiwa na malengo ya kuzalisha wahitimu wabunifu, wenye uwezo na wepesi ambao watakuwa na athari katika shughuli za uongezaji thamani madini hapa nchini.

 

MADINI NI MAISHA NA UTAJIRI

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals