Tarehe : Nov. 5, 2024, 5:25 p.m.
●Kujengwa kwa miezi 27
●Barrick kufadhili kwa asilimia 100
KAHAMA
Imeelezwa kwamba Kampuni ya uchimbaji wa madini ya dhahabu ya Barrick inaendelea na utekelezaji wa ujenzi wa Barabara ya Kahama hadi Bulyanhulu yenye urefu wa kilomita 73.9 kwa kiwango cha lami itakayogharimu kiasi shilingi zaidi ya bilioni 100.
Hayo yalielezwa hivi karibuni na Meneja wa Kampuni ya Barrick nchini Tanzania Melkiory Ngido wakati akizungumza katika mkutano na vyombo vya habari kuhusu Mpango wa Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo yenye ubia na Serikali ya Tanzania.
Akielezea kuhusu faida zitakazopatikana pindi mradi huo utakapo kamilika , Ngido alieleza kuwa wananchi wa Wilaya ya Kahama watapata fursa ya kusafirisha na kushiriki maendeleo ya kiuchumi pamoja na kusafiri kwa wepesi katika kutafuta huduma muhimu.
Ngido alieleza kwamba, pamoja na ujenzi wa barabara hiyo , tayari kampuni ya Barrick imetumia zaidi ya shilingi bilioni mbili katika ujenzi wa miundombinu ya barabara ikiwemo mitaro ya maji katika kijiji cha Kakola na Bushingwe na ujenzi wa Chuo cha Ufundi cha VETA cha Bunango, miradi ya afya na elimu katika vijiji vinavyozunguka mgodi Bulyanhulu
Naye , Mwenyekiti wa kijiji cha Ilogi Edward Shija alisema kuwa utekelezaji wa mradi huo umeanza vizuri kwa kuwashirikisha wananchi kuanzia hatua za awali ambapo kukamilika kwa barabara hiyo kutawezesha wananchi kufika kwa haraka katika maeneo mengine yanayoungana na wilaya ya Kahama na vitongoji vyake ili kupata huduma mbalimbali ikiwemo Biashara , Afya na Elimu.
by: madini
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…
by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…
by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.
’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…
by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…
by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.