[Latest Updates]: Waziri wa Madini Akemea Utoroshaji wa Madini Geita

Tarehe : May 29, 2022, 9:29 a.m.
left

Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko amesema licha ya kuwepo kwa jitihada za Vyombo vya Ulinzi na Usalama, uanzishwaji wa masoko na kufutwa kwa tozo mbalimbali lakini bado kuna baadhi ya watu wasio waaminifu wanatorosha madini.

Dkt. Biteko ameyasema hayo wakati akizungumza na wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu katika eneo la Lwamgasa mkoani Geita ambapo amewataka waachane na tabia ya kutorosha madini na badala yake wayapeleke sokoni.

Aidha, Dkt. Biteko amewataka wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu pamoja na watanzania wote kushirikiana na Vyombo vya Ulinzi na Usalama ili kuwabainisha watoroshaji wa madini nchini.

Dkt. Biteko amesema madini ya dhahabu yanayotokana na Mialo hayaonekani sokoni ambapo amesema kuna uwezekano mkubwa kwamba dhahabu inayo chenjuliwa kwenye Mialo inatoroshwa. 

Katika hatua nyingine, Dkt. Biteko amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan anatamani kuona watanzania wanabadili maisha yao kupitia Sekta ya Madini.

"Saa ya nyinyi kufanya kazi na kutajirika ni sasa, Mama yetu Mhe. Samia Suluhu Hassan anatamani kutuona wachimbaji wadogo wa madini tunatajirika na tunabadilisha maisha yetu kupitia uchimbaji wa madini," amesema Dkt. Biteko.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Geita Rosemary Senyamule amesema Mkoa wake anajipanga kuandaa mazingira yatakayopelekea kuujenga mkoa huo kuwa kitovu cha madini ya dhahabu Afrika ambapo mikoa mingine na nchi za jirani watajifunza kupitia mkoa huo. 

"Tunatamani Mkoa wetu wa Geita kuwa kitovu cha madini ya dhahabu sio tu kwa Tanzania bali Afrika kwa ujumla," amesema Senyamule.

Pia, Senyamule amesema mkoa wa Geita umeanza kujenga majengo ya kudumu kwa ajili ya Maonyesho ya Teknolojia na Uwekezaji katika Sekta Madini ili yawe na hadhi ya kimataifa.

 

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals