[Latest Updates]: Umeme Kuongeza Uzalishaji wa Madini Mkoa wa Katavi - Mavunde

Tarehe : July 15, 2024, 3:56 p.m.
left

Katavi

Waziri wa Madini Mh . Anthony Mavunde amewaeleza wachimbaji wa mkoa wa Katavi kwamba utekelezaji wa mradi wa kuingiza Katavi kwenye gridi ya Taifa itasaidia upataikanaji wa uhakika wa umeme na hivyo kupelekea kuongezeka kwa uzalishaji wa madini mkoani Katavi.

Waziri Mavunde aliyasema hayo jana Julai14, 2024 Mpanda, Mkoani Katavi wakati wa kikao cha pamoja kati yake na uwakilishi wa wachimbaji mkoani Katavi ikiwa ni muendelezo wa ziara ya kikazi ya Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia S. Hassan mkoani humo.

“Tunaishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Mh. Rais Dkt. Samia S. Hassan kwa utekelezaji mkubwa wa mradi wa umeme ambao umelenga kuuingiza mkoa wa Katavi kwenye gridi ya Taifa na hivyo kusaidia upatikanaji wa umeme wa uhakika" alisema Mhe.Mavunde

Mhe.Mavunde aliongeza kuwa baada ya Katavi kuingia kwenye gridi ya Taifa,uzalishaji wa madini utaongezeka maradufu kuliko hivi sasa na hivyo kupelekea kuongezeka kwa mapato yatokanayo na sekta ya madini.

Kuhusu suala la tozo zinazongezeka mara kwa mara kupitia Mamlaka za Halmashauri za Wilaya na Manispaa, tutakutana na Waziri wa TAMISEMI ili tulizungumze hili kwa pamoja na kulipatia muafaka jambo hili”Alisema Mavunde

Akitoa salamu za wachimbaji , Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wachimba Madini Mkoa wa Katavi (KATAREMA) Ndg. William Mbogo ameishukuru Serikali na Mh. Rais Dkt. Samia S. Hassan kwa utashi wake wa kukuza sekta ya madini nchini kwa kuiongezea Bajeti Wizara ya Madini kufikia Tsh 231bn ili kusaidia kufanya utafiti wa kina nchi nzima  kwa lengo la kuwawezesha wachimbaji wadogo kuchimba bila  kubahatisha.

Aidha, Mbogo amemuomba Waziri wa Madini kushughulikia matatizo yaliyowasilishwa ikiwemo suala la upatikanaji wa nishati ya umeme wa uhakika na tozo zilizokithiri zilizotambulishwa na Halmashauri za Wilaya na Manispaa ambazo zinakwenda  kuathiri suala la uchimbaji kwa kiasi kikubwa.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals