[Latest Updates]: Usawa wa Kijinsia Wasisitizwa Taasisi za Serikali na Binafsi

Tarehe : March 9, 2023, 12:30 p.m.
left

Taasisi zote za Serikali na binafsi zimesisitizwa kuwepo kwa usawa wa kijinsia mahala pa kazi hususan katika shughuli zote za maendeleo ikiwemo nafasi za maamuzi, siasa na umiliki wa mali ikiwemo ardhi.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambayo kimkoa yamefanyika wilaya ya Kondoa.

Aidha, Senyamule amesema mkoa wa Dodoma unajumla ya idadi ya watu 3,083,625 ambapo wanawake ni asilimia 51 na wanaume asilimia 49 ambapo mikakati ya Serikali ni kuona ifikapo 2030 nafasi ya mwanamke iwe imefikia asilimia 50 kwa 50 katika masuala mbalimbali yakiwemo masuala ya maamuzi na maendeleo ya kiuchumi.

Senyamule amesema lengo la kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani ni kutaka kuhamasisha jamii juu ya uwezo wa wanawake katika kuleta Usawa wa Kijinsia na maendeleo ya kiuchumi.

Katika hatua nyingine, Senyamule amesema wanawake ni Jeshi kubwa wakiwezeshwa wanaweza na wamesisitizwa kuepuka vishawishi vya kuingia kwenye ndoa za jinsia moja.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Maadhimisho ya Mkoa wa Dodoma, Penina Robert amesema amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kwa kuwawezesha wanawake kupata mikopo ya riba nafuu na amewaomba wanawake kote nchini kuungana kwenye vikundi ili kuepuka mikopo umiza.

Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani huadhimishwa kila mwaka tarehe 8, Machi, mwaka huu 2023  yamebebwa na Kaulimbiu isemayo "Ubunifu na Mabadiliko ya Teknolojia Chachu katika kuleta Usawa wa Kijinsia" ambapo zaidi ya Taasisi 97 kutoka mkoa wa Dodoma zimeshiriki.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals