[Latest Updates]: Mwenyekiti wa Bodi ya EITI Mhe. Helen Clark Afanya Ziara Nchini Tanzania

Tarehe : April 3, 2024, 2:03 p.m.
left

-Kukutana na Rais Samia Suluhu Hassan 

Kuelekea hatua muhimu ya Uwazi na Uwajibikaji katika Sekta ya Uchimbaji Nchini, Mwenyekiti wa Asasi ya Bodi ya Kimataifa ya Uhamasishaji Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali za Madini, Mafuta na Gesi Asilia (EITI), Mhe. Helen Clark, amewasili Tanzania kwa ziara muhimu ya siku sita hapa nchini, kuanzia leo Aprili 3 hadi Aprili 8, 2024.

Ziara hiyo ni hatua muhimu katika kuimarisha usimamizi wa rasilimali hizo hapa nchini, ili kufikia viwango vya ubora wa kimataifa unaotakiwa katika usimamizi wa rasilimali Pamoja na kuimarisha ushirikiano baina ya EITI na TEITI.

Baada ya kuwasili, Mhe. Helen Clark alipokelewa na ujumbe wa Tanzania, ukiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Madini Kheri Mahimbali Mwenyekiti wa Kamati ya Taasisi ya Uhamasishaji Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali za Madini, Mafuta na Gesi Asilia Tanzania (TEITI) CPA. Ludovick Utouh, Mwakilishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Noel Kaganda Pamoja na Kaimu Katibu Mtendaji wa TEITI Mariam Mgaya.

Akiwa katika ziara yake hapa nchini, Mhe. Helen Clark anatarajiwa kuwa na mikutano na majadiliano ya kimkakati ambapo pia atakutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, tarehe 4 Aprili, 2024, ambapo kunatarajiwa kuwa majadiliano ya msingi yatakayoimarisha azma ya Tanzania katika kuongeza uwazi na uwajibikaji katika Usimamizi wa Rasilimali za Madini, Mafuta na Gesi Asilia zilizopo hapa nchini.

Mbali na majadiliano ya kiserikali, Mhe. Helen Clark pia atakutana na wadau mbalimbali wanaohusika katika Sekta hiyo hapa nchini kwa lengo la kujadiliana kuhusu changamoto na fursa za utekelezaji wa kanuni na taratibu za EITI, kujadili njia bora ya pamoja katika kuhamasisha uwazi na uwajibikaji katika usimamizi wa rasilimali hizo.

Matarajio ya ziara hiyo ni kuisaidia Tanzania kuimarisha usimamizi bora wa rasilimali zake za madini, mafuta pamoja na gesi asilia sambamba na kuisaidia Tanzania kufikia viwango vya kimataifa katika usimamizi wa uwazi na uwajibikaji, na kuendelea kuwa mfano kwa mataifa mengine katika usimamizi wa rasilimali hizo.

Mhe. Helen Clark, amewahi kuwa Waziri Mkuu wa New Zealand, lakini pia amewahi kuhudumu kama Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Mipango ya Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals