[Latest Updates]: Wabunge Waipongeza Menejimenti ya Mgodi wa North Mara Kutekeleza Mpango wa CSR

Tarehe : Feb. 21, 2024, 8:20 p.m.
left

●Mwaka 2023 Madarasa 396 kati ya 1090 yamejengwa

●Mabweni 97 kati ya 280 yalijengwa

●Asilimia 96 ya wafanyakazi wa mgodi ni watanzania

●Asilimia 86 ya manunuzi yameenda  kwa wafanyabiashara wa ndani

Mara

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wameupongeza Mgodi wa North Mara kwa kutelekeza Dhana ya Uwajibikaji wa Kampuni kwa jamii inayozunguka mgodi (CSR) hususani katika miradi ya maendeleo ikiwemo Elimu, Afya na Maji mkoani humo.

Hayo yamebainishwa leo Februari  21,2024 na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Nishati na Madini, Mathayo David Mathayo mkoani Mara  wakati wa ziara ya kutembelea Mgodi wa North mara kwa lengo la kuangalia miradi ya maendeleo na kupata taarifa ya  maendeleo ya mgodi huo. 

Akizungumza wakati akitoa taarifa ya majumuisho ya ziara kwa wajumbe wa Kamati na menejimenti ya Mgodi, mwenyekiti Mathayo  ameupongeza mgodi huo kwa kuweza kuzingatia mpango wa CSR katika kutekeleza miradi ya maendeleo kwa sekta ya Elimu , Afya na Maji katika maeneo mbalimbali yanayozunguka  mgodi.

Pia, Mwenyekiti ameupongeza mgodi kwa kutengeneza Bwawa kubwa  la maji taka (TFS) ambalo linatumia mifumo mizuri ya kisasa katika kudhibiti utunzaji wa maji taka yanayotoka mgodini.

Naye , Naibu Waziri wa Madini Dkt.Steven Kiruswa ameutaka mgodi kufanya tafiti za madini katika maeneo mengine yaliyo karibu na mgodi na kuwapatia wachimbaji wadogo ili nao wajihusishe na uchimbaji ili kujenga uhusiano mzuri baina ya mgodi na  wananchi wanaozunguka  mgodi huo.

Akitoa taarifa ya maendeleo ya mgodi , Meneja Mkuu wa Mgodi wa huo Apolinary Lyambiko amesema kuwa  mgodi  umekuwa kinara katika ulipaji wa kodi  na  hadi sasa kiasi cha Tshs.3.25 trilioni zimelipwa kama kodi.

Lyambiko ameongeza kuwa asilimia 96 ya wafanyakazi wa mgodi ni watanzania, huku asilimia 86 ya manunuzi ndani  ya mgodi zinakuwa kwa wafanyabiashara wadogo na watoa huduma, huku asilimia 70 za manunuzi zinaend kwa kampuni za ndani ya nchi.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals