[Latest Updates]: Tanzania Kinara wa Uwekezaji Mkubwa wa Madini kwa Kampuni Kutoka Australia

Tarehe : Sept. 4, 2024, 5:05 p.m.
left

-Asilimia 21 ya uwekezaji wa Kampuni kubwa za Madini za Australia Barani Afrika ni nchini Tanzania

-Kampuni zaingia mikataba ya uwekezaji wa zaidi ya Trilioni 10

-Miradi mipya kuongeza Mapato, Ajira na ushiriki wa watanzania

-Rais Dkt. Samia apongezwa kufungua uwekezaji

-Waziri Mavunde asisitiza manufaa ya uwekezaji huo kwa maendeleo ya Watanzania

Perth,Australia

Tanzania imetajwa kuwa nchi kinara kwa Bara la Afrika ambayo kampuni za Madini za Australia zimewekeza kwa asilimia 21% ya uwekezaji wote wa kwenye Sekta ya Madini.

Hayo yameelezwa leo Perth, Australia wakati wa mkutano wa Africa DownUnder(ADU) unaowashirikisha wadau wa madini kutoka Australia na Nchi za Bara la Afrika.

Akihutubia mkutano huo kwa niaba ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu  Hassan, Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde amesema mikataba ya madini iliyoingiwa kwa miaka miwili iliyopita baina ya Kampuni za Madini za Australia na Serikali ya Tanzania ina thamani ya zaidi ya Shilingi Trilioni Kumi na hivyo utekelezaji wake utasaidia kuongeza mapato ya nchi,kuongeza nafasi za ajira,ushiriki wa watanzania(Local Content) na kuchochea ukuajinwa sekta ya madini.

Aidha,Waziri Mavunde alizitaka kampuni hizo kuheshimu mikataba waliyoingina na serikali na hasa katika kunufaisha watanzania kupitia wajibu kwa jamii(CSR),utoaji huduma na usambazaji wa bidhaa migodini na ulipaji wa kodi na tozo stahiki ili rasilimali hizo zitoe mchango katika maendeleo ya uchumi wa nchi na watu wake.

Wakitoa mawasilisho yao Watendaji wa Kampuni za Chief , Walkabout Resources,Peak Rare Earths, Black Rock Mining  na Eco Graf kwa pamoja wameipongeza serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Mh. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji na hivyo kuvutia uwekezaji huu mkubwa nchini ambao utachochea kukuaji wa kasi wa uchumi wa Tanzania.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals