[Latest Updates]: STAMICO Yadhamiria Kuwawezesha Wachimbaji Wadogo wa Madini

Tarehe : June 25, 2024, 10:52 p.m.
left

Dodoma

Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limeelezea Mipango yake ikiwemo kuendelea kuwawezesha Wachimbaji Wadogo wa Madini nchini, huku msisitizo ukiwekwa kwenye ununuzi wa mitambo na huduma za uchorongaji ili kuwasaidia kupata taarifa za miamba, hatimaye wachimbe kwa tija.

Hayo yalielezwa  Juni 24, 2024 na Meneja Uwezeshaji Uchimbaji Mdogo kutoka STAMICO Bw. Tuna Bandoma kwenye Wiki ya Madini inayokwenda sambamba na Kongamano la Wachimba Madini, Mkutano wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji wa Madini Tanzania (FEMATA) pamoja na  maonesho ya madini na vifaa vya uchimbaji inayoendelea katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Convention Center jijini Dodoma.

Aliongeza kwamba, mitambo hiyo itawahudumia zaidi wachimbaji wadogo wenye leseni hai huku akitaja huduma hiyo kutumia gharama ndogo ambazo itamhitaji mchimbaji kuchangia, ambazo ni nafuu ikilinganishwa na uhalisia wa gharama za uchorongaji.

Akizungumzia mgawanyo wa mitambo hiyo, Bandoma alisema ugawaji wake umezingatia maeneo yenye idadi kubwa ya shughuli za uchimbaji mdogo ikiwemo Mkoa wa Geita na uwepo wa miradi ya mashirika makubwa ili kusaidia  kuhifadhi mitambo hiyo.

Vilevile, akizungumzia kuhusu uwezeshaji wa kifedha, Bandoma alisema STAMICO itaendelea kuimarisha taarifa za wachimbaji wadogo ili waweze kuaminika na kukopesheka na taasisi za fedha.

Naye, Muhasibu kutoka FEMATA Bw. Gregory Kibusi alitumia fursa hiyo kuipongeza STAMICO kwa kuendelea kuwa karibu na wachimbaji wadogo katika kuwawezesha kujiinua kiuchumi kupitia mitambo ya uchorongaji.

STAMICO imeendelea kutekeleza  majukumu  yake ya kuwasimamia  na kuwaendeleza  wachimbaji wadogo  kwa kutoa elimu ya uchimbaji bora unaotumia teknolojia ya kisasa, kuandaa mikutano  inayowakutanisha na wadau wa ndani na nje ya nchi pamoja na kuleta mitambo  ya uchorongaji maalum  kwao inayowasaidia kujua kiwango cha rasilimali  katika maeneo yao ya uchimbaji.


#InvestIntanzaniaMiningSector

#Vision2030: MadininiMaisha&Utajiri

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals