[Latest Updates]: Maafisa madini watakiwa kuwa wabunifu, ukusanyaji maduhuli

Tarehe : Nov. 29, 2018, 10:03 a.m.
left

Na Greyson Mwase, Lindi

Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa Nchini wametakiwa kuongeza ubunifu kwenye  ukusanyaji wa mapato ili kuweza kufikia lengo lililowekwa na Serikali hivyo Sekta ya Madini kuwa na mchango mkubwa kwenye ukuaji wa uchumi wa nchi.

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni inayojihusisha na uchimbaji wa kokoto ya Drumax Construction kwa kushirikiana na kampuni inayomilikiwa na Said Seif iliyopo katika Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara, George Tayyar (kulia) akielezea changamoto za kampuni yake kwa Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (kushoto) mara alipofanya ziara kwenye machimbo hayo.[/caption]

Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 13 Desemba, 2018 na Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo kwenye kikao chake na watumishi wa Ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Lindi iliyopo Wilayani Nachingwea mkoani Lindi ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku mbili kwenye mkoa huo, yenye lengo la kukagua shughuli za uchimbaji wa madini pamoja na kutatua kero mbalimbali.

Naibu Waziri Nyongo aliyekuwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Rukia Mhango alisema kuwa, Serikali kupitia Wizara ya Madini imeweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha kuwa Sekta ya Madini inakuwa na mchango mkubwa kwenye ukuaji wa sekta nyingine kutokana na makusanyo ya kodi mbalimbali za madini.

“Ninawaagiza maafisa madini wakazi kuhakikisha wanafikia lengo lililowekwa na Serikali kwenye ukusanyaji wa kodi mbalimbali zitokanazo na Sekta ya Madini kwa kuwa wabunifu, na tupo tayari kusaidia pale itakapowezekana,” alisema Naibu Waziri Nyongo.

Katika hatua nyingine, Nyongo aliwataka maafisa madini kujiridhisha na maeneo yanayoombewa leseni kabla ya kutoa leseni  ili kuepusha migogoro inayoweza kujitokeza kati ya wamiliki wa leseni na wananchi wanaozunguka maeneo ya uchimbaji.

Wakati huohuo akizungumza mara baada ya kuhitimisha ziara yake kwenye kiwanda cha uzalishaji wa saruji cha Dangote kilichopo mkoani Mtwara, Naibu Waziri Nyongo alisema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Madini  imeweka mazingira mazuri ya uwekezaji kwenye sekta ya madini na kusisitiza kuwa Serikali ipo tayari kutoa ushirikiano kwa wawekezaji ili waweze kuzalisha zaidi na Serikali kupata mapato yake stahiki.

Aidha, Naibu Waziri alifanya ziara katika machimbo ya kokoto yanayomilikiwa na kampuni za Drumax Construction na Said Seff na  kiwanda cha kutengeneza vyombo vya ibada kwa kutumia madini ya mawe kinachomilikiwa na Shirika la Benedictine Abbey katika Wilaya ya Masasi na kuwahakikishia watendaji wake kuwa Serikali imejipanga katika kutatua changamoto zinazowakabili ili uwekezaji wao uwe na manufaa, hivyo kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi wa nchi.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals