Tarehe : June 22, 2024, 2:47 p.m.
Bodi ya EITI yaridhia Kikao cha Bodi kufanyika Tanzania
Ushirikiano wa EITI na Tanzania kuimarishwa
Bodi ya Asasi ya Kimataifa ya (Extractive Industries Transparency Iniative - EITI) tarehe 18 - 20 Juni, 2024 ilifanya kikao chake cha 60 huko Geniva, Switzerland ambapo imeazimia kufanya Kikao chake cha Bodi ya Asasi hiyo nchini Tanzania mapema mwakani 2025 ambapo Mkutano huo umepangwa kufanyika Jijini Arusha.
Maamuzi hayo yamefanyika ikiwa ni miezi michache tu Mwenyekiti wa Bodi hiyo Retired Helen Clark pamoja na ujumbe wake walivyowasilia nchini kwa ziara Mwezi Aprili 2024 ambapo Mwenyekiti wa Bodi hiyo alifanya vikao mbalimbali na wadau kujadili utekelezaji wa shughuli za EITI hapa.
Aidha Bi.Helen Clark alikutana na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko na Waziri wa Madini Mhe. Antony Peter Mavunde, Kamati ya TEITI, Asasi za Kiraia na Makampuni ya Madini, Mafuta na Gesi Asilia.
Moja ya mambo muhimu yaliyozungumzwa ni Wizara ya Madini ikishirikiana na Asasi za Kimataifa ya EITI kutimiza kikamilifu mahitaji ya matakwa ya Kimataifa ya Uwazi na Uwajibikaji katika shughuli mbalimbali za Usimamizi wa Rasilimali Madini, Mafuta na Gesi Asilia nchini.
"Amesisitiza dhana ya kuweka uwazi taarifa na takwimu mbalimbali juu ya Sekta ya Uziduaji ni kuhakikisha kuwa Rasilimali hizo zinawanufaisha wananchi na kuahidi kuwa TEITI itatoa ushirikiano katika kutekeleza Matakwa hayo".
Mapendekezo ya Kufanyika kwa Mkutano wa Bodi ya EITI ni kielelezo cha kuimarika kwa Uwazi na Uwajibikaji katika usimamizi wa Rasilimali Madini, Mafuta na Gesi Asilia hapa nchini.
Mkutano huo utahudhuriwa na wajumbe zaidi 50 ikijumuishwa na Mwenyekiti wa Bodi Rt. Helen Clark, Sekretariati ya Asasi ya Kimataifa ya EITI na waalikwa mbalimbali kutoka nchi mbalimbali duniani.
by: madini
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…
by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…
by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.
’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…
by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…
by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.