Tarehe : Sept. 30, 2023, 9:54 a.m.
• *Kuandaa Mkakati wa Uwezeshaji Wanawake*
• *Kupewa leseni za maeneo yenye taarifa za Utafiti*
Serikali kupitia Wizara ya Madini na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wanawake na Makundi Maalum leo Septemba 29 ,2023 imepokea changamoto zinazowakabili wachimbaji madini wanawake katika maadhimisho ya miaka 25 ya Chama Cha Wachimbaji Wanawake Tanzania ( TAWOMA).
Akizungumza katika maadhimisho hayo Mwenyekiti wa TAWOMA Semeni Malale amesema katika kipindi cha miaka 25 TAWOMA imekuwa ikikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa leseni za uchimbaji , kutokuwa na vifaa vya uchimbaji , kukosa mitaji pamoja na kutokopesheka katika Taasisi za Fedha.
Semeni amefafanua kuwa TAWOMA inakosa fursa nyingi ndani ya sekta ya madini kutokana nguvu yake ya kiuchumi kuwa ndogo katika mnyororo mzima wa madini.
Akizungumza katika maadhimisho hayo Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde amesema kuwa Serikali inatambua changamoto zenu hivyo kupitia Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) litakabidhi mitambo 5 mitano kwa wachimbaji wadogo kwa ajili ya uchorongaji itakayowasaidia katika kufanya utafiti wa kina ili waweze kuchimbaji kwa uhakika.
Sambamba na hapo Mhe. Mavunde ameongeza kuwa kupitia VISION 2030 ya Madini ni Maisha na Utajiri upo mpango wa kuwapatia leseni 15 kwa vikundi vya watu 20 ambapo zitatolewa pindi STAMICO itakapomaliza kuandaa utaratibu.
Kwa upande wake Dkt. Dorothy Gwajima Waziri wa Maendeleo ya Jamii , Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum amesema Serikali ya Awamu ya Sita inatoa nafasi kubwa kwa wanawake hususani katika Sekta za Uchumi , hivyo kupitia vyama vya wachimbaji madini wanawake kama vile TAWOMA imepanga kuwajengea uwezo kwa kuwakutanishi na Taasisi za fedha ili kujadiliana namna bora ya kupata mikopo yenye riba nafuu kwa shughuli za uchimbaji madini.
Aidha , akielezea kuhusu mafanikio Malale amesema mpaka sasa TAWOMA imefanikiwa kuratibu mafunzo mbalimbali kwa wanachama ndani na nje ya nchi yanayohusu Afya,Usimamizi mahala pa kazi , utunzaji mazingira katika uchimbaji ,uongezaji thamani madini na biashara ya rasilimali madini.
TAWOMA ilianzishwa mwaka 1997 mpaka sasa ina wanachama zaidi 4000 katika mikoa 21 ikiwa na lengo la kufikia Mikoa yote na kufikisha wanachama zaidi 10000 ifikapo mwaka 2025.
|
by: madini
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…
by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…
by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.
’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…
by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…
by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.