[Latest Updates]: Wizara ya Madini Yaweka Mikakati Mipya kwa Klabu Yake ya Michezo

Tarehe : Oct. 17, 2023, 8:28 a.m.
left

# Yaibuka na Medali Nne SHIMIWI

# Medali za Fedha 2, Shaba 1 na Dhahabu 1

Katika kuhakikisha Klabu ya Michezo ya Madini ( Madini Sports Club) inashiriki michezo kwa mafanikio makubwa   imebainisha mikakati ya kiufundi itakayo leta matokeo bora  katika michezo.

Mikakati hiyo  imebainishwa leo Oktoba 17 , 2023 na Naibu Katibu Mkuu Madini Msafiri Mbibo alipomwakilisha Katibu Mkuu Madini katika kikao cha  kupokea taarifa ya ushiriki  wa Mashindano ya Shirikisho la Michezo  la Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI - 2023) jijini Dodoma.

Mbibo amesema kuwa Wizara imefurahishwa na ushindi mlioupata katika mashindano ya SHIMIWI lakini pamoja na ushindi huo Wizara ina mikakati mbalimbali ya kiufundi ikiwemo mpango wa  kushiriki  michezo  mbalimbali katika ngazi ya mkoa na taifa kwa lengo la  kuwajengea uwezo wanamichezo wote.

Mbibo aliongeza kuwa Wizara ina mpango wa kuwa na eneo maalum kwa ajili ya kufanya mazoezi litakalojumuisha michezo yote pamoja na kuwepo na vifaa vyote vya michezo ili wanamichezo wa klabu ya madini waweze kupata uzoefu kabla ya kuingia katika mashindano.

Sambamba na hayo Mbibo amefafanua kuwa katika michezo motisha ni vyenzo muhimu ya ushindi hivyo Wizara itaendelea kutoa motisha kwa wanamichezo wote kwa jinsi itakavyowezekana nia kubwa ni kutoa hamasa kwa  wanamichezo.

Awali akitoa taarifa ya ushiriki Mwenyekiti wa Klabu ya Michezo ya Madini John Issangu amesema kuwa klabu ya madini ilishiriki kwa ushindani mkubwa na kuweza kupata medali nne  ikiwamo ya Dhahabu moja, medali za fedha mbili na Shaba moja.

Akielezea juu ya ushindi huo Issangu amesema Medali hizo zilipatikana katika mchezo wa riadha kuanzia Mbio za mita 100 kwa washiriki kuanzia umri wa miaka 55-60 , medali ya fedha ilipatikana katika Mbio za mita 200 , medali ya tatu ambayo ya fedha ilipatikana  katika  mita 800 na medali katika mita 400.

Mashindano ya SHIMIWI ujumuhisha michezo mbalimbali ukiwemo mchezo wa mpira wa miguu, mpira wa Pete, kurusha tufe , mbio za baiskeli na michezo ya ndani kama vile Bao ,Draft na Karata.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals