[Latest Updates]: Serikali Kuwawezesha Vifaa Vijana Wahitimu wa Fani ya Uongezaji Thamani Madini

Tarehe : Nov. 16, 2023, 4:27 p.m.
left

Serikali ya Awamu ya Sita imedhamiria kuhakikisha panakuwepo na mwendelezo wa ujuzi na utaalam wanaopata wanafunzi wa fani ya jemolojia ambapo imepanga kuwapatia bure vifaa vya kuwawezesha kujiajiri na kuongeza thamani ya madini.

Hayo yamesemwa leo tarehe 17 Novemba, 2023 Jijini Arusha na Waziri wa Madini, Mheshimiwa Anthony Peter Mavunde (Mb) alipotembelea Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC) kinachotoa mafunzo ya Astashahada na Stashahada ya fani za Jemolojia na uongezaji wa thamani madini.

" Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alipokuwa ziarani Mkoani Lindi, alituelekeza Wizara ya Madini kuhakikisha tunaweka mkazo katika uongezaji thamani madini. Katika kutekeleza hilo, Kituo hiki ni muhimu sana katika kuwezesha Serikali kufanikisha uongezaji wa thamani madini nchini." amesema Mhe. Mavunde 

"Ili kuondokana na changamoto inayowakabili wahitimu wengi wa Kituo cha TGC, kuanzia mwaka ujao wa fedha 2024/2025 Serikali kupitia Wizara ya Madini itatenga fedha za kuwezesha vifaa kwa vijana wanaohitimu ili waweze kujiajiri na kuwa na mchango katika uongezaji thamani madini nchini." ameongeza Mhe. Mavunde 

Serikali isingependa kuona vijana wanaohitimu katika fani ya Jemolojia na uongezaji thamani madini, wanakwenda kufanya shughuli zingine kwa changamoto kubwa tu ya kukosa mitaji au vifaa vya kuwezesha kutumia ujuzi wao.

Uwezeshwaji wa vifaa kwa vijana hao itakuwa ni sehemu ya utekelezaji wa Programu ya kuwezesha vijana kwenye sekta ya madini itayojulikana kama Mining for a Brighter Tommorow (MBT) yenye lengo la kuongeza ushiriki wa vijana kwenye shughuli zote za mnyororo wa thamani wa madini”Alisema Mavunde

Awali, akimkaribisha Mheshimiwa Waziri, Kamishna wa Madini, Dkt. AbdulRahman Mwanga alibainisha kuwa Kituo hicho kimedhamiria kuhakikisha kwamba dhamira ya Serikali katika uongezaji thamani madini nchini hususan ya Vito inakwenda kutimia.

Naye Kaimu Mratibu wa Kituo cha TGC, Bw. Jumanne Shimba aliipongeza na kuishukuru Serikali kupitia Wizara ya Madini kwa namna inavyowezesha Kituo hicho, ikiwa ni pamoja na kuanza kwa ujenzi wa jengo jipya la kisasa ambalo hatua za manunuzi zimeanza kama hatua za mwisho za kuanza ujenzi wake.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals